ترجمة معاني القرآن الكريم - الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس

سورة الضحى - Ad-Duha

external-link copy
1 : 93

وَٱلضُّحَىٰ

Mwenyezi Mungu Anaapa kwa wakati wa dhuha, na uliokusudiwa ni wakati wa mchana mzima. info
التفاسير:

external-link copy
2 : 93

وَٱلَّيۡلِ إِذَا سَجَىٰ

Na kwa usiku utuliapo na viumbe na likashadidi giza lake. Mwenyezi Mungu Huapa kwa Atakacho katika viumbe vyake. Ama kiumbe, hafai kuapa kwa asiyekuwa Muumba wake. Kuapa kwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu ni ushirikina. info
التفاسير:

external-link copy
3 : 93

مَا وَدَّعَكَ رَبُّكَ وَمَا قَلَىٰ

Hakukuwacha Mola wako, ewe Mtume, wala Hakukuchukia kwa kuchelewesha kukuteremshiaWahyi. info
التفاسير:

external-link copy
4 : 93

وَلَلۡأٓخِرَةُ خَيۡرٞ لَّكَ مِنَ ٱلۡأُولَىٰ

Na Nyumba ya Akhera ni bora kwako kuliko nyumba ya ulimwengu. info
التفاسير:

external-link copy
5 : 93

وَلَسَوۡفَ يُعۡطِيكَ رَبُّكَ فَتَرۡضَىٰٓ

Na Atakupa Mola wako, ewe Mtume, neema ya kila sampuli uridhike. info
التفاسير:

external-link copy
6 : 93

أَلَمۡ يَجِدۡكَ يَتِيمٗا فَـَٔاوَىٰ

Kwani Hakukupata, kabla ya hapo, kuwa ni yatima Akakukusanya na kukutunza. info
التفاسير:

external-link copy
7 : 93

وَوَجَدَكَ ضَآلّٗا فَهَدَىٰ

Na Akakupata hujui Kitabu wala Imani, Akakufundisha yale amabayo ulikuwa huyajui na akakuafikia kufanya amali bora? info
التفاسير:

external-link copy
8 : 93

وَوَجَدَكَ عَآئِلٗا فَأَغۡنَىٰ

Na Akakupata masikini, Akakuletea riziki yako na Akakutajirisha kwa kutosheka na kusubiri? info
التفاسير:

external-link copy
9 : 93

فَأَمَّا ٱلۡيَتِيمَ فَلَا تَقۡهَرۡ

Basi yatima usimtende ubaya. info
التفاسير:

external-link copy
10 : 93

وَأَمَّا ٱلسَّآئِلَ فَلَا تَنۡهَرۡ

Na muombaji usimkaripie, bali mlishe na umtimizie haja yake. info
التفاسير:

external-link copy
11 : 93

وَأَمَّا بِنِعۡمَةِ رَبِّكَ فَحَدِّثۡ

Na ama neema ya Mola wako Aliyokuneemesha nayo izungumze. info
التفاسير: