Onjeni ukali wa Moto huu. Vumilieni uchungu wake na ukali wake au msiyavumilie hayo, hamtahafifishiwa adhabu na hamtatoka humo. Ni sawasawa kwenu nyinyi mkivumilia au mkitovumilia. Hakika nyinyi mnalipwa tu yale mliokuwa mkiyafanya duniani.
التفاسير:
17:52
إِنَّ ٱلۡمُتَّقِينَ فِي جَنَّٰتٖ وَنَعِيمٖ
Hakika wachamungu watakuwa kwenye mabustani ya Pepo na neema kubwa.
Watajistarehesha kwa vile Alivyowapa Mwenyezi Mungu vya neema miongoni mwa aina mbalimbali za ladha na starehe, na Atawaokoa mwenyezi Mungu kutokana na adhabu ya Moto.
Na wale walioamini na wakafuatwa na watoto wao katika hiyo Imani, Tutawakutanisha watoto wao nao katika daraja yao Peponi, hata kama hawakufikia matendo ya wazazi wao, ili wazazi wafurahike na watoto wao pamoja na wao katika daraja zao. Watakusanywa baina yao kwenye hali nzuri zaidi, na hatutawapunguzia chochote katika matendo yao mema. Kila mtu anafungwa na matendo yake aliyoyachuma, hatobeba dhambi za watu wengine..
Na miongoni mwa starehe hizo ni kuwa wao watapeana gilasi ya pombe, mmoja wao atampa mwenzake, ili furaha yao ikamilike. Kinywaji hiki kinatafautiana na pombe ya duniani, hakimleweshi akili mwenye kukinywa, wala hakisababishi kubobokwa, wala maneno ya makosa na maasia.
Na watawazunguka watumishi waliotayarishwa kuwatumikia kama kwamba wao katika usafi na weupe na utungaji nidhamu ni lulu iliyohifadhiwa kwenye mashaza yake.
Watasema, «Sisi tulikuwa kabla, huko duniani, na sisi tuko baina ya watu wetu, tunamuogopa Mola wetu, tuna hadhari na adhabu Yake na mateso yake Siku ya Kiyama.
Mwenyezi Mungu Akatuneemesha kwa uongofu na taufiki na Akatuokoa na adhabu ya vuke la Jahanamu, nalo ni moto wake na joto lake. Sisi tulikuwa, hapo kabla, tukimnyenyekea Yeye Peke Yake, hatumshirikishi na Yeye yoyote asiyekuwa Yeye, Atulinde na adhabu ya vuke la Motoni na Atupeleke kwenye starehe ya Peponi.
Mwenyezi Mungu Akatukubalia maombi yetu, na Akatupa tulichokiomba. Hakika Yeye Ndiye Mwingi wa kheri, Mwenye kurehemu. Na miongoni mwa wingi wa kheri Zake na rehema Zake kwetu ni kule kutupa radhi zake na Pepo, na kutuepusha na hasira Zake na Moto.»
Basi wawaidhie, ewe Mtume, wale uliotumilizwa kwao kwa Qur’ani, kwani hukuwa wewe, kwa neema ya Mwenyezi Mungu Aliokuneemesha kwayo ya unabii na busara ya akili, ni kuhani anayetoa habari za ghaibu bila ujuzi wala mwendawazimu asiyejua analolisema, kama wanavyodai.