ترجمة معاني القرآن الكريم - الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس

external-link copy
51 : 23

يَٰٓأَيُّهَا ٱلرُّسُلُ كُلُواْ مِنَ ٱلطَّيِّبَٰتِ وَٱعۡمَلُواْ صَٰلِحًاۖ إِنِّي بِمَا تَعۡمَلُونَ عَلِيمٞ

Enyi Mitume! Kuleni riziki ya halali na fanyeni matendo mema, kwani mimi kwa mnayoyafanya ni mjuzi, hakuna kitu chochote chenye kufichika kwangu katika matendo yenu. Wanaohutubiwa katika aya hii ni Mitume wote kwa jumla, amani iwashukie, na wafuasi wao. Na katika aya pana dalili kwamba kula halali inasaidia kufanya matendo mema na kwamba mwisho wa haramu ni mbaya na miongoni mwa ubaya wake ni kurudishwa dua kwa kutokubaliwa. info
التفاسير: