《古兰经》译解 - 斯瓦希里语翻译-阿里·穆哈森·伯瓦尼

页码:close

external-link copy
5 : 63

وَإِذَا قِيلَ لَهُمۡ تَعَالَوۡاْ يَسۡتَغۡفِرۡ لَكُمۡ رَسُولُ ٱللَّهِ لَوَّوۡاْ رُءُوسَهُمۡ وَرَأَيۡتَهُمۡ يَصُدُّونَ وَهُم مُّسۡتَكۡبِرُونَ

Na wanapo ambiwa: Njooni ili Mtume wa Mwenyezi Mungu akuombeeni maghfira, huvigeuza vichwa vyao, na unawaona wanageuka nao wamejaa kiburi. info

Na wakiambiwa: Jongeeni, apate Mtume wa Mwenyezi Mungu kukuombeeni msamaha, hutikisa vichwa vyao kwa kejeli, na utawaona wanageuka kwa kiburi hawataki kut'ii.

التفاسير:

external-link copy
6 : 63

سَوَآءٌ عَلَيۡهِمۡ أَسۡتَغۡفَرۡتَ لَهُمۡ أَمۡ لَمۡ تَسۡتَغۡفِرۡ لَهُمۡ لَن يَغۡفِرَ ٱللَّهُ لَهُمۡۚ إِنَّ ٱللَّهَ لَا يَهۡدِي ٱلۡقَوۡمَ ٱلۡفَٰسِقِينَ

Sawa sawa kwao, ukiwatakia maghfira au hukuwatakia maghfira, Mwenyezi Mungu hatawaghufiria. Hakika Mwenyezi Mungu hawaongoi watu wapotovu. info

Ni sawa kwa hawa wanaafiki, ukiwaombea msamaha, au ukito waombea. Kwa sababu hao hawauachi unaafiki wao. Basi Mwenyezi Mungu hatawasamehe kabisa. Hakika Mwenyezi Mungu hawaongozi kuwapeleka kwenye Haki wale wanao kataa kufuata amri yake na kumuamini.

التفاسير:

external-link copy
7 : 63

هُمُ ٱلَّذِينَ يَقُولُونَ لَا تُنفِقُواْ عَلَىٰ مَنۡ عِندَ رَسُولِ ٱللَّهِ حَتَّىٰ يَنفَضُّواْۗ وَلِلَّهِ خَزَآئِنُ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِ وَلَٰكِنَّ ٱلۡمُنَٰفِقِينَ لَا يَفۡقَهُونَ

Hao ndio wanao sema: Msitoe mali kwa ajili ya walioko kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu, ili waondokelee mbali! Na Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye khazina za mbingu na ardhi, lakini wanaafiki hawafahamu. info

Hao wanaafiki ndio wanao waambia watu wa Madina: Msitoe chochote kuwapa hao Waumini walio na Mtume wa Mwenyezi Mungu ili wapate kumwacha! Na Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye khazina zote za mbinguni na duniani, na riziki zote ziliomo humo. Lakini wanaafiki hawajui hayo.

التفاسير:

external-link copy
8 : 63

يَقُولُونَ لَئِن رَّجَعۡنَآ إِلَى ٱلۡمَدِينَةِ لَيُخۡرِجَنَّ ٱلۡأَعَزُّ مِنۡهَا ٱلۡأَذَلَّۚ وَلِلَّهِ ٱلۡعِزَّةُ وَلِرَسُولِهِۦ وَلِلۡمُؤۡمِنِينَ وَلَٰكِنَّ ٱلۡمُنَٰفِقِينَ لَا يَعۡلَمُونَ

Wanasema: Tukirejea Madina mwenye utukufu zaidi bila ya shaka atamfukuza aliye mnyonge. Na Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye utukufu - Yeye, na Mtume wake, na Waumini. Lakini wanaafiki hawajui. info

Wanaafiki wanasema kwa kutoa ahadi: Tukirejea Madina hapana shaka kikundi chetu, ambacho ndicho chenye nguvu zaidi, kitakitoa kikundi cha Waumini ambao ni wanyonge! Nguvu anazo Mwenyezi Mungu, na Mtume wake, na Waumini; sio hawa wanao jitia kuahidi. Lakini wanaafiki hawajui kitu.

التفاسير:

external-link copy
9 : 63

يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ لَا تُلۡهِكُمۡ أَمۡوَٰلُكُمۡ وَلَآ أَوۡلَٰدُكُمۡ عَن ذِكۡرِ ٱللَّهِۚ وَمَن يَفۡعَلۡ ذَٰلِكَ فَأُوْلَٰٓئِكَ هُمُ ٱلۡخَٰسِرُونَ

Enyi mlio amini! Yasikusahaulisheni mali yenu, wala watoto wenu, kumkumbuka Mwenyezi Mungu. Na wenye kufanya hayo ndio walio khasiri. info

Enyi mlio msadiki Mwenyezi Mungu na Mtume wake! Yasikuhangaisheni mali yenu, na watoto wenu, hata mkaacha kumkumbuka Mwenyezi Mungu na kutekekeleza aliyo kuamrisheni kuyafanya. Na wenye kushughulishwa na mali zao na watoto wao wakaacha hayo, basi hao ndio watao kuwa wamekhasiri Siku ya Kiyama.

التفاسير:

external-link copy
10 : 63

وَأَنفِقُواْ مِن مَّا رَزَقۡنَٰكُم مِّن قَبۡلِ أَن يَأۡتِيَ أَحَدَكُمُ ٱلۡمَوۡتُ فَيَقُولَ رَبِّ لَوۡلَآ أَخَّرۡتَنِيٓ إِلَىٰٓ أَجَلٖ قَرِيبٖ فَأَصَّدَّقَ وَأَكُن مِّنَ ٱلصَّٰلِحِينَ

Na toeni katika tulicho kupeni kabla hayajamfikia mmoja wenu mauti, tena hapo akasema: Mola wangu Mlezi! Huniakhirishi muda kidogo nipate kutoa sadaka, na niwe katika watu wema? info

Enyi Waumini! Toeni katika mali tuliyo kuruzukuni upesi upesi kabla mmoja wenu hayajamfikia mauti akasema kwa majuto: Ewe Mola wangu Mlezi! Hebu hunipi muhula kidogo, nikapata kutoa sadaka, na nikawa miongoni wa watu wema watendao vitendo vyema?

التفاسير:

external-link copy
11 : 63

وَلَن يُؤَخِّرَ ٱللَّهُ نَفۡسًا إِذَا جَآءَ أَجَلُهَاۚ وَٱللَّهُ خَبِيرُۢ بِمَا تَعۡمَلُونَ

Wala Mwenyezi Mungu hataiakhirisha nafsi yoyote inapo fika ajali yake; na Mwenyezi Mungu anazo khabari za mnayo yatenda. info

Wala Mwenyezi Mungu hampi muhula mtu yeyote ukisha fika wakati wake wa kufa. Na Mwenyezi Mungu ni Mkamilifu wa kujua yote myatendayo, na Yeye atakulipeni kwa hayo.

التفاسير: