《古兰经》译解 - 斯瓦希里语翻译 - 阿布杜拉·穆罕默德和纳赛尔·海米斯。

external-link copy
142 : 7

۞ وَوَٰعَدۡنَا مُوسَىٰ ثَلَٰثِينَ لَيۡلَةٗ وَأَتۡمَمۡنَٰهَا بِعَشۡرٖ فَتَمَّ مِيقَٰتُ رَبِّهِۦٓ أَرۡبَعِينَ لَيۡلَةٗۚ وَقَالَ مُوسَىٰ لِأَخِيهِ هَٰرُونَ ٱخۡلُفۡنِي فِي قَوۡمِي وَأَصۡلِحۡ وَلَا تَتَّبِعۡ سَبِيلَ ٱلۡمُفۡسِدِينَ

Mwenyezi Mungu, kutakasika na sifa za upungufu ni Kwake na kutukuka ni Kwake, Alimpa ahadi Mūsā ya kuzungumza na Mola wake masiku thelathini, kisha Akamuengezea muda wa masiku kumi baada yake, ukakamilika wakati ambao Mwenyezi Mungu Alimuwekea Mūsā wa kusema na Yeye kuwa masiku arubaini. Na Mūsā alisema kumwambia ndugu yake Hārūn, alipotaka kwenda kuzungumza na Mola wake, «Kuwa ni badala yangu kwa watu wangu mpaka nitakaporudi, na uwahimize wamtii Mwenyezi Mungu na wamuabudu, na usifuate njia ya wale ambao wanaleta uharibifu katika ardhi.» info
التفاسير: