《古兰经》译解 - 斯瓦希里语翻译 - 阿布杜拉·穆罕默德和纳赛尔·海米斯。

external-link copy
129 : 7

قَالُوٓاْ أُوذِينَا مِن قَبۡلِ أَن تَأۡتِيَنَا وَمِنۢ بَعۡدِ مَا جِئۡتَنَاۚ قَالَ عَسَىٰ رَبُّكُمۡ أَن يُهۡلِكَ عَدُوَّكُمۡ وَيَسۡتَخۡلِفَكُمۡ فِي ٱلۡأَرۡضِ فَيَنظُرَ كَيۡفَ تَعۡمَلُونَ

Walisema watu wa Mūsā, miongoni mwa Wana wa Isrāīl, kumwambia Nabii wao Mūsā, «Tulisumbuliwa na tukaudhiwa na nguvu za Fir'awn na watu wake, kwa kuuawa watoto wetu wa kiume na kuachiliwa wanawake wetu, kabla hujatujia na baada ya kutujia.» Mūsā akawaambia, «Huenda Mola wenu Akamuangamiza adui yenu, Fir'awn na watu wake, na Awaweke nyinyi katika ardhi yao badala yao, baada ya kuangamia kwao, Aangalie namna mtakavyofanya: mtashukuru au mtakufuru?» info
التفاسير: