《古兰经》译解 - 斯瓦希里语翻译 - 阿布杜拉·穆罕默德和纳赛尔·海米斯。

页码:close

external-link copy
44 : 7

وَنَادَىٰٓ أَصۡحَٰبُ ٱلۡجَنَّةِ أَصۡحَٰبَ ٱلنَّارِ أَن قَدۡ وَجَدۡنَا مَا وَعَدَنَا رَبُّنَا حَقّٗا فَهَلۡ وَجَدتُّم مَّا وَعَدَ رَبُّكُمۡ حَقّٗاۖ قَالُواْ نَعَمۡۚ فَأَذَّنَ مُؤَذِّنُۢ بَيۡنَهُمۡ أَن لَّعۡنَةُ ٱللَّهِ عَلَى ٱلظَّٰلِمِينَ

Watu wa Peponi, baada ya kuingia humo, watawaita watu wa Motoni wawaambie, «Sisi tumeshapata kuwa ni kweli tuliyoahidiwa na Mola wetu, kupitia ndimi za Mitume Wake, kuhusu kuwalipa wanaomtii. Je, nyinyi mumeyapata mliyoahidiwa na Mola wenu, kupitia ndimi za Mitume Wake, kuwa ni kweli kuhusu kuwaadhibu wanaomuasi?» Hapo watu wa Motoni watawajibu watu wa Peponi wakiwaambia, «Ndio, kwa kweli tumeyapata yale Aliyotuahidi Mola wetu kuwa ni kweli.» Hapo Atatangaza mwenye kutangaza, akiwa kati baina ya watu wa Peponi na watu wa Motoni akisema, «Laana ya Mwenyezi Mungu iwashukie watu madhalimu» ambao walikiuka mipaka ya Mwenyezi Mungu na wakamkanusha Mwenyezi Mungu na Mtume Wake. info
التفاسير:

external-link copy
45 : 7

ٱلَّذِينَ يَصُدُّونَ عَن سَبِيلِ ٱللَّهِ وَيَبۡغُونَهَا عِوَجٗا وَهُم بِٱلۡأٓخِرَةِ كَٰفِرُونَ

Makifiri hawa ndio wale waliokuwa wakiipuuza njia ya Mwenyezi Mungu iliyolingana sawa, na wakiwazuia watu wasiifuate, na wakitaka kwamba njia ya kuifuata iwe kombo ili kusiwe na yoyote wa kuielewa; na wao, kuhusu Akhera na mambo yake, ni wenye kukanusha. info
التفاسير:

external-link copy
46 : 7

وَبَيۡنَهُمَا حِجَابٞۚ وَعَلَى ٱلۡأَعۡرَافِ رِجَالٞ يَعۡرِفُونَ كُلَّۢا بِسِيمَىٰهُمۡۚ وَنَادَوۡاْ أَصۡحَٰبَ ٱلۡجَنَّةِ أَن سَلَٰمٌ عَلَيۡكُمۡۚ لَمۡ يَدۡخُلُوهَا وَهُمۡ يَطۡمَعُونَ

Na baina ya watu wa Peponi na watu Motoni patakuwa na kizuizi kikubwa kinaitwa Al-A’rāf. Na juu ya kizuizi hiki kutakuwa na wanaume wanaowajuwa watu wa Peponi na watu wa Motoni kwa alama zao kama weupe wa nyuso za watu wa Peponi na weusi wa nyuso za watu wa Motoni. Wanaume hawa ni watu ambao vitendo vyao vizuri na viovu viko sawasawa, na wao wana matumaini ya kupata rehema ya Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka. Wanaume hao wa hapo Al-A’rāf watawaita watu wa Peponi kwa maamkuzi wakiwaambia, «Salamun 'alaykum»(Amani iwe juu yenu.) Watu hawa wa Al-A’rāf bado hawajaingia Peponi, na wao wana matumaini ya kuingia. info
التفاسير:

external-link copy
47 : 7

۞ وَإِذَا صُرِفَتۡ أَبۡصَٰرُهُمۡ تِلۡقَآءَ أَصۡحَٰبِ ٱلنَّارِ قَالُواْ رَبَّنَا لَا تَجۡعَلۡنَا مَعَ ٱلۡقَوۡمِ ٱلظَّٰلِمِينَ

Na yatakapogeuzwa macho ya watu wa Al-A’rāf upande wa watu wa Motoni watasema, «Ewe Mola wetu, usitufanye kuwa pamoja na watu madhalimu» kwa ya ushirikina wao na ukafiri wao. info
التفاسير:

external-link copy
48 : 7

وَنَادَىٰٓ أَصۡحَٰبُ ٱلۡأَعۡرَافِ رِجَالٗا يَعۡرِفُونَهُم بِسِيمَىٰهُمۡ قَالُواْ مَآ أَغۡنَىٰ عَنكُمۡ جَمۡعُكُمۡ وَمَا كُنتُمۡ تَسۡتَكۡبِرُونَ

Na watu walioko Al-A’rāf watawaita wanaume, miongoni mwa viongozi wa makafiri waliomo motoni, wanaowajua kwa alama zao fulani zinazowatenganisha wawaambie, «Hayakuwafaa chochote mali mliokuwa mkiyakusanya ulimwenguni wala watu; pia hakikuwafaa kiburi chenu kilichowafanya nyinyi msimuamini Mwenyezi Mungu na msiikubali haki.» info
التفاسير:

external-link copy
49 : 7

أَهَٰٓؤُلَآءِ ٱلَّذِينَ أَقۡسَمۡتُمۡ لَا يَنَالُهُمُ ٱللَّهُ بِرَحۡمَةٍۚ ٱدۡخُلُواْ ٱلۡجَنَّةَ لَا خَوۡفٌ عَلَيۡكُمۡ وَلَآ أَنتُمۡ تَحۡزَنُونَ

Je madhaifu na mafukara hawa, kati ya watu wa Peponi, ndio wale mlioapa huko duniani kwamba Mwenyezi Mungu Hatawakusanya Siku ya Kiyama Awatie kwenye rehema na Hatawaingiza Peponi? Ingieni Peponi, enyi watu wa Al- A'rāf, hakika mumesamehewa; hamna tene kicho cha kupata adhabu ya Mwenyezi Mungu, wala hamtahuzunika juu ya hadhi za duniani zilizowapita. info
التفاسير:

external-link copy
50 : 7

وَنَادَىٰٓ أَصۡحَٰبُ ٱلنَّارِ أَصۡحَٰبَ ٱلۡجَنَّةِ أَنۡ أَفِيضُواْ عَلَيۡنَا مِنَ ٱلۡمَآءِ أَوۡ مِمَّا رَزَقَكُمُ ٱللَّهُۚ قَالُوٓاْ إِنَّ ٱللَّهَ حَرَّمَهُمَا عَلَى ٱلۡكَٰفِرِينَ

Watu wa Motoni wataomba msaada kwa watu wa Peponi wawamiminie maji au chakula Mwenyezi Mungu Alichowaruzuku. Na wao watawajibu kwamba Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, Ameviharamisha vinywaji na vyakula kwa walioukanusha upweke Wake na wakawafanya Mitume Wake kuwa ni warongo. info
التفاسير:

external-link copy
51 : 7

ٱلَّذِينَ ٱتَّخَذُواْ دِينَهُمۡ لَهۡوٗا وَلَعِبٗا وَغَرَّتۡهُمُ ٱلۡحَيَوٰةُ ٱلدُّنۡيَاۚ فَٱلۡيَوۡمَ نَنسَىٰهُمۡ كَمَا نَسُواْ لِقَآءَ يَوۡمِهِمۡ هَٰذَا وَمَا كَانُواْ بِـَٔايَٰتِنَا يَجۡحَدُونَ

Wale ambao Mwenyezi mungu, Aliyetukuka, Atawanyima starehe za Akhera ni wale ambao waliifanya Dini, ambayo Mwenyezi Mungu Amewaamuru kuifuata, kuwa ni pumbao, na yakawadanganya wao maisha ya ulimwenguni, wakashughulishwa na mapambo yake wasifanye matendo ya kuwafaa Akhera, hao Atawasahau Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, Siku ya Kiyama, na Atawaacha ndani ya adhabu iumizayo, kama walivyoyaacha matendo ya kuwafaa kwa kukutana na Siku yao hii, na kwa kuwa wao walikuwa wakizikanusha dalili za Mwenyezi Mungu na hoja Zake pamoja na kujua kwao kuwa ni za ukweli. info
التفاسير: