《古兰经》译解 - 斯瓦希里语翻译 - 阿布杜拉·穆罕默德和纳赛尔·海米斯。

external-link copy
76 : 6

فَلَمَّا جَنَّ عَلَيۡهِ ٱلَّيۡلُ رَءَا كَوۡكَبٗاۖ قَالَ هَٰذَا رَبِّيۖ فَلَمَّآ أَفَلَ قَالَ لَآ أُحِبُّ ٱلۡأٓفِلِينَ

Giza la usiku lilipomuingilia Ibrāhīm, amani imshukiye, na kumfinika, alijadiliana na watu wake ili kuwathibitishia kuwa dini yao ni ya urongo. Na wao walikuwa wakiabudu nyota. Ibrāhīm, amani imshukiye, aliona nyota, akasema, akiwavuta watu wake, ili awathibitishie tawhīd (upweke wa Mwenyezi Mungu) kihoja, «Hii ni mola wangu.» Nyota ilipozama alisema, «Mimi siwapendi waungu wanaozama.» info
التفاسير: