《古兰经》译解 - 斯瓦希里语翻译 - 阿布杜拉·穆罕默德和纳赛尔·海米斯。

external-link copy
63 : 6

قُلۡ مَن يُنَجِّيكُم مِّن ظُلُمَٰتِ ٱلۡبَرِّ وَٱلۡبَحۡرِ تَدۡعُونَهُۥ تَضَرُّعٗا وَخُفۡيَةٗ لَّئِنۡ أَنجَىٰنَا مِنۡ هَٰذِهِۦ لَنَكُونَنَّ مِنَ ٱلشَّٰكِرِينَ

Waambie, ewe Mtume, hawa washirikina, «Ni nani mwenye kuwaokoa na vitisho vya magiza ya bara na bahari? Kwani si Mwenyezi Mungu mnayemuomba kwenye matatizo mkionesha unyonge wenu kwa dhahiri na kwa siri? Huwa mkisema, ‘Hakika Mola wetu Akituokoa na vitisho hivi, tutakuwa ni wenye kushukuru kwa kumuabudu, Aliyeshinda na kutukuka, Peke Yake, Asiye na mshirika.» info
التفاسير: