《古兰经》译解 - 斯瓦希里语翻译 - 阿布杜拉·穆罕默德和纳赛尔·海米斯。

external-link copy
58 : 6

قُل لَّوۡ أَنَّ عِندِي مَا تَسۡتَعۡجِلُونَ بِهِۦ لَقُضِيَ ٱلۡأَمۡرُ بَيۡنِي وَبَيۡنَكُمۡۗ وَٱللَّهُ أَعۡلَمُ بِٱلظَّٰلِمِينَ

Sema, ewe Mtume, «Lau mimi nina mamlaka ya kuwateremshia adhabu ambayo mnaitaka kwa haraka, ningaliiteremsha kwenu, na uamuzi, baina yangu mimi na nyinyi, ungalitoka. Lakini hilo liko kwa Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka. Na Yeye Anawajua zaidi madhalimu ambao wamepita mipaka yao wakawashirikisha wengine pamoja na Yeye. info
التفاسير: