《古兰经》译解 - 斯瓦希里语翻译 - 阿布杜拉·穆罕默德和纳赛尔·海米斯。

external-link copy
32 : 6

وَمَا ٱلۡحَيَوٰةُ ٱلدُّنۡيَآ إِلَّا لَعِبٞ وَلَهۡوٞۖ وَلَلدَّارُ ٱلۡأٓخِرَةُ خَيۡرٞ لِّلَّذِينَ يَتَّقُونَۚ أَفَلَا تَعۡقِلُونَ

Maisha ya kilimwengu hayakuwa, katika wingi wa hali zake, isipokuwa ni udanganyifu na ubatilifu. Na matendo mema, kwa kutengeneza nyumba ya Akhera, ndiyo bora kwa wenye kumcha Mwenyezi Mungu, wakajikinga na adhabu Yake kwa kumtii na kujiepusha na mambo ya kumuasi. Kwani hamuelewi, enyi washirikina mlioghurika na pambo la uhai wa kilimwengu, mukayatanguliza yanayosalia mbele ya yanayomalizika? info
التفاسير: