《古兰经》译解 - 斯瓦希里语翻译 - 阿布杜拉·穆罕默德和纳赛尔·海米斯。

页码:close

external-link copy
82 : 6

ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ وَلَمۡ يَلۡبِسُوٓاْ إِيمَٰنَهُم بِظُلۡمٍ أُوْلَٰٓئِكَ لَهُمُ ٱلۡأَمۡنُ وَهُم مُّهۡتَدُونَ

Wale waliomuamini Mwenyezi Mungu na Mtume Wake na wakafuata sheria Yake kivitendo, na wasichanganye imani yao na ushirikina, wao ndio wenye utulivu na usalama na wao ndio walioongozwa kwenye njia ya haki. info
التفاسير:

external-link copy
83 : 6

وَتِلۡكَ حُجَّتُنَآ ءَاتَيۡنَٰهَآ إِبۡرَٰهِيمَ عَلَىٰ قَوۡمِهِۦۚ نَرۡفَعُ دَرَجَٰتٖ مَّن نَّشَآءُۗ إِنَّ رَبَّكَ حَكِيمٌ عَلِيمٞ

Hoja hiyo ambayo Ibrāhīm, amani imshukiye, aliwahoji nayo watu wake ndiyo hoja yetu tuliyomuongoza nayo mpaka hoja yao ikakatika. Tunamtukuza daraja tunayemtaka, miongoni mwa waja wetu, ulimwenguni na Akhera, Hakika Mola wako ni Mwenye hekima katika kuendesha mambo ya waja Wake, ni Mjuzi kuhusu wao. info
التفاسير:

external-link copy
84 : 6

وَوَهَبۡنَا لَهُۥٓ إِسۡحَٰقَ وَيَعۡقُوبَۚ كُلًّا هَدَيۡنَاۚ وَنُوحًا هَدَيۡنَا مِن قَبۡلُۖ وَمِن ذُرِّيَّتِهِۦ دَاوُۥدَ وَسُلَيۡمَٰنَ وَأَيُّوبَ وَيُوسُفَ وَمُوسَىٰ وَهَٰرُونَۚ وَكَذَٰلِكَ نَجۡزِي ٱلۡمُحۡسِنِينَ

Na tulimneemesha Ibrāhīm, amani imshukiye, kwa kumruzuku Is’ḥāq kuwa mtoto wake na Ya‘qūb kuwa mjukuu. Na wote wawili tuliwaongoza kwenye njia ya uongofu. Pia tulimuongoza Nūḥ kwenye haki, kabla ya Ibrāhīm na Isḥāq na Ya’qūb. Na pia tuliwaongoza kwenye haki, kati ya kizazi cha Nūḥ, Dāwūd, Sulaimān, Ayyūb, Yūsuf, Mūsā na Hārūn, amani iwashukie. Na kama tulivyowajazi Manabii hawa kwa wema wao, ndivyo tunavyomjazi kila mwema. info
التفاسير:

external-link copy
85 : 6

وَزَكَرِيَّا وَيَحۡيَىٰ وَعِيسَىٰ وَإِلۡيَاسَۖ كُلّٞ مِّنَ ٱلصَّٰلِحِينَ

Na vilivile tulimuongoza Zakariyyā, Yaḥyā, ‘Īsā na Ilyās. Na Manabii wote hawa, amani iwashukie, ni miongoni mwa watu wema. info
التفاسير:

external-link copy
86 : 6

وَإِسۡمَٰعِيلَ وَٱلۡيَسَعَ وَيُونُسَ وَلُوطٗاۚ وَكُلّٗا فَضَّلۡنَا عَلَى ٱلۡعَٰلَمِينَ

Na tulimuongoza, vilevile, Ismā‘īl, Ilyasa‘ na Lūṭ,. Na Mitume wote hawa tuliwatukuza juu ya watu wa zama zao. info
التفاسير:

external-link copy
87 : 6

وَمِنۡ ءَابَآئِهِمۡ وَذُرِّيَّٰتِهِمۡ وَإِخۡوَٰنِهِمۡۖ وَٱجۡتَبَيۡنَٰهُمۡ وَهَدَيۡنَٰهُمۡ إِلَىٰ صِرَٰطٖ مُّسۡتَقِيمٖ

Na pia tuliwaongoza kwenye haki tuliowataka kuwaongoza kati ya wazazi wa hawa, watoto wao na ndugu zao. Na tuliwateua wao wafuate Dini yetu na wafikishe ujumbe wetu kwa wale tuliowatuma kwao. Na tuliwaonesha njia sahihi, isiyopotoka, nayo ni ile ya kumpwekesha Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, na kumwepusha na mambo ya kumshirkisha.. info
التفاسير:

external-link copy
88 : 6

ذَٰلِكَ هُدَى ٱللَّهِ يَهۡدِي بِهِۦ مَن يَشَآءُ مِنۡ عِبَادِهِۦۚ وَلَوۡ أَشۡرَكُواْ لَحَبِطَ عَنۡهُم مَّا كَانُواْ يَعۡمَلُونَ

Uongofu huo ni taufiki ya Mwenyezi Mungu ambayo kwayo Anamuongoza Anayemtaka miongoni mwa waja Wake. Na lau hawa Manabii walimshirikisha Mwenyezi Mungu, kwa kuchukulia na kukadiria, amali zao zingalipomoka. Kwani Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, Hakubali amali yoyote pamoja na ushirikina. info
التفاسير:

external-link copy
89 : 6

أُوْلَٰٓئِكَ ٱلَّذِينَ ءَاتَيۡنَٰهُمُ ٱلۡكِتَٰبَ وَٱلۡحُكۡمَ وَٱلنُّبُوَّةَۚ فَإِن يَكۡفُرۡ بِهَا هَٰٓؤُلَآءِ فَقَدۡ وَكَّلۡنَا بِهَا قَوۡمٗا لَّيۡسُواْ بِهَا بِكَٰفِرِينَ

Manabii hao tuliowaneemesha kwa uongofu na unabii, ndio wale tuliowapa Kitabu, kama vile kurasa za Ibrāhīm, Taurati ya Muūsā, Zaburi ya Dāwūd na Injili ya Īsā. Na tuliwapa ufahamu wa Vitabu hivi na tukawateua kufikisha wahyi wetu. Na iwapo makafiri wa watu wako, ewe Mtume, watazikanusha aya za hii Qur’ani, basi tumewategemezea watu wengine jambo hilo, - yaani: Muhājirūn (masahaba waliohamia Madina pamoja na Mtume) na Ans,ār (masahaba wenyeji wa Madina) na wafuasi wao mpaka Siku ya Kiyama- ambao hawatakuwa ni wenye kuzikanusha. Bali watakuwa ni wenye kuziamini, ni wenye kuzitumia. info
التفاسير:

external-link copy
90 : 6

أُوْلَٰٓئِكَ ٱلَّذِينَ هَدَى ٱللَّهُۖ فَبِهُدَىٰهُمُ ٱقۡتَدِهۡۗ قُل لَّآ أَسۡـَٔلُكُمۡ عَلَيۡهِ أَجۡرًاۖ إِنۡ هُوَ إِلَّا ذِكۡرَىٰ لِلۡعَٰلَمِينَ

Manabii hao waliotajwa ndio ambao Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, Amewaongoza kwenye dini Yake ya haki. Basi fuata uongofu wao, ewe Muhammad, na andama njia yao. Waambie washirikina, «Mimi sitaki kutoka kwenu, kwa kufikisha Uislamu, badala ya ulimwengu. Malipo yangu yako kwa Mwenyezi Mungu. Na Uislamu ni kuita watu wote kwenye njia iliyolingana sawa na ni ukumbusho kwenu na kwa kila aliyekuwa kama nyinyi, kati ya wale wanaoendelea kwenye batili; huenda nyinyi mkawaidhika nao mkanufaika. info
التفاسير: