《古兰经》译解 - 斯瓦希里语翻译 - 阿布杜拉·穆罕默德和纳赛尔·海米斯。

Al-Mujadilah

external-link copy
1 : 58

قَدۡ سَمِعَ ٱللَّهُ قَوۡلَ ٱلَّتِي تُجَٰدِلُكَ فِي زَوۡجِهَا وَتَشۡتَكِيٓ إِلَى ٱللَّهِ وَٱللَّهُ يَسۡمَعُ تَحَاوُرَكُمَآۚ إِنَّ ٱللَّهَ سَمِيعُۢ بَصِيرٌ

Ashasikia Mwenyezi Mungu neno la Khawalah binti ya Tha’labah anayekurudiarudia kuhusu mumewe Aws mwana wa al-Ṣāmit na kuhusu kile kilichotokea upande wake cha kufanya ẓihār nako ni kule kutamka mumewe kumwambia yeye, «wewe kwangu mimi ni kama mgongo wa mamangu», yaani katika uharamu wa kumuingilia, na huku anamnyenyekea Mwenyezi Mungu Aliyetukuka Amtatulie shida yake, na Mwenyezi Mungu Anayasikia maneno yenu na marudiano yenu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Msikizi wa kila neno, ni Muoni wa kila kitu, hakifichiki Kwake chochote chenye kufichika. info
التفاسير: