《古兰经》译解 - 斯瓦希里语翻译 - 阿布杜拉·穆罕默德和纳赛尔·海米斯。

external-link copy
7 : 5

وَٱذۡكُرُواْ نِعۡمَةَ ٱللَّهِ عَلَيۡكُمۡ وَمِيثَٰقَهُ ٱلَّذِي وَاثَقَكُم بِهِۦٓ إِذۡ قُلۡتُمۡ سَمِعۡنَا وَأَطَعۡنَاۖ وَٱتَّقُواْ ٱللَّهَۚ إِنَّ ٱللَّهَ عَلِيمُۢ بِذَاتِ ٱلصُّدُورِ

Na kumbukeni neema ya Mwenyezi Mungu kwenu katika sheria Yake Aliyowaekea na kumbukeni ahadi Yake Yeye Aliyetukuka, Aliyoichukua kwenu ya kumuamini Mwenyezi Mungu na Mtume Wake Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, kuwasikiliza na kuwatii. Na mcheni Mwenyezi Mungu katika Aliyowaamrisha na Aliyowakataza. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa mnayoyaficha katika nafsi zenu. info
التفاسير: