《古兰经》译解 - 斯瓦希里语翻译 - 阿布杜拉·穆罕默德和纳赛尔·海米斯。

external-link copy
4 : 5

يَسۡـَٔلُونَكَ مَاذَآ أُحِلَّ لَهُمۡۖ قُلۡ أُحِلَّ لَكُمُ ٱلطَّيِّبَٰتُ وَمَا عَلَّمۡتُم مِّنَ ٱلۡجَوَارِحِ مُكَلِّبِينَ تُعَلِّمُونَهُنَّ مِمَّا عَلَّمَكُمُ ٱللَّهُۖ فَكُلُواْ مِمَّآ أَمۡسَكۡنَ عَلَيۡكُمۡ وَٱذۡكُرُواْ ٱسۡمَ ٱللَّهِ عَلَيۡهِۖ وَٱتَّقُواْ ٱللَّهَۚ إِنَّ ٱللَّهَ سَرِيعُ ٱلۡحِسَابِ

Wanakuuliza Maswahaba wako, ewe Nabii, «Ni kipi walichohalalishiwa kukila?» Waambie, «Mumehalalishiwa kula vilivyo vizuri na viwindwa vya wanyama mliowafundisha kati ya wanyama wanaowinda kwa kutumia makucha na meno yao, miongoni mwa mbwa, chui na kozi na kama hao kati ya wale wanaofundishwa. Mnawafundisha kuwatafutia viwindwa kwa yale Mwenyezi Mungu Aliyowafundisha. Basi kuleni wanyama waliowashikia na mlitaje jina la Mwenyezi Mungu wakati mnapowatuma kuwawindia. Na muogopeni Mwenyezi Mungu katika yale Aliyowaamrisha na yale Aliyowakataza.» Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwepesi wa kuhesabu. info
التفاسير: