《古兰经》译解 - 斯瓦希里语翻译 - 阿布杜拉·穆罕默德和纳赛尔·海米斯。

页码:close

external-link copy
14 : 5

وَمِنَ ٱلَّذِينَ قَالُوٓاْ إِنَّا نَصَٰرَىٰٓ أَخَذۡنَا مِيثَٰقَهُمۡ فَنَسُواْ حَظّٗا مِّمَّا ذُكِّرُواْ بِهِۦ فَأَغۡرَيۡنَا بَيۡنَهُمُ ٱلۡعَدَاوَةَ وَٱلۡبَغۡضَآءَ إِلَىٰ يَوۡمِ ٱلۡقِيَٰمَةِۚ وَسَوۡفَ يُنَبِّئُهُمُ ٱللَّهُ بِمَا كَانُواْ يَصۡنَعُونَ

Na tulichukua ahadi ya mkazo kwa wale waliodai kuwa wao ni wafuasi wa Al-Masīḥ ‘Īsā mwana wa Maryam, na hali wao sio hivyo, kama ile tulioichukua kwa Wana wa Isrāīl, kwamba watamfuata Mtume wao, watamnusuru na watamsaidia, lakini walibadilisha Dini yao na wakaacha kutumia sehemu ya yale waliyokumbushwa nayo, kama walivyofanya Mayahudi. Kwa hivyo tulitia uadui na chuki kati yao mpaka Siku ya Kiyama. Na Mwenyezi Mungu Atawapa habari, Siku ya Hesabu, ya yale ambayo wao walikuwa wakiyafanya, na Atawatesa kwa matendo yao. info
التفاسير:

external-link copy
15 : 5

يَٰٓأَهۡلَ ٱلۡكِتَٰبِ قَدۡ جَآءَكُمۡ رَسُولُنَا يُبَيِّنُ لَكُمۡ كَثِيرٗا مِّمَّا كُنتُمۡ تُخۡفُونَ مِنَ ٱلۡكِتَٰبِ وَيَعۡفُواْ عَن كَثِيرٖۚ قَدۡ جَآءَكُم مِّنَ ٱللَّهِ نُورٞ وَكِتَٰبٞ مُّبِينٞ

Enyi watu mliopewa Kitabu , miongoni mwa Mayahudi na Wanaswara! Amewajia nyinyi mjumbe wetu Muhammad , rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, kuwafafanulia mengi ambayo mlikuwa mkiyaficha kwa watu katika yale yaliyomo ndani ya Taurati na Injili, na kuacha kuyafafanua yale ambayo busara haitaki yafafanuliwe. Hakika umewajia kutoka kwa Mwenyezi Mungu mwngaza na Kitabu chenye ufafanuzi, nacho ni Qur’ani tukufu. info
التفاسير:

external-link copy
16 : 5

يَهۡدِي بِهِ ٱللَّهُ مَنِ ٱتَّبَعَ رِضۡوَٰنَهُۥ سُبُلَ ٱلسَّلَٰمِ وَيُخۡرِجُهُم مِّنَ ٱلظُّلُمَٰتِ إِلَى ٱلنُّورِ بِإِذۡنِهِۦ وَيَهۡدِيهِمۡ إِلَىٰ صِرَٰطٖ مُّسۡتَقِيمٖ

Kwa kitabu hiki chenye ufafanuzi, Mwenyezi Mungu Anawaongoza wenye kufuata yenye kumridhi Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, njia za amani na usalama, Anawatoa kutoka kwenye giza la ukafiri kuwapeleka kwenye mwangaza wa Imani na Anawaafikia wao kufuata dini Yake iliyolingana sawa. info
التفاسير:

external-link copy
17 : 5

لَّقَدۡ كَفَرَ ٱلَّذِينَ قَالُوٓاْ إِنَّ ٱللَّهَ هُوَ ٱلۡمَسِيحُ ٱبۡنُ مَرۡيَمَۚ قُلۡ فَمَن يَمۡلِكُ مِنَ ٱللَّهِ شَيۡـًٔا إِنۡ أَرَادَ أَن يُهۡلِكَ ٱلۡمَسِيحَ ٱبۡنَ مَرۡيَمَ وَأُمَّهُۥ وَمَن فِي ٱلۡأَرۡضِ جَمِيعٗاۗ وَلِلَّهِ مُلۡكُ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِ وَمَا بَيۡنَهُمَاۚ يَخۡلُقُ مَا يَشَآءُۚ وَٱللَّهُ عَلَىٰ كُلِّ شَيۡءٖ قَدِيرٞ

Kwa hakika wamekufuru Wanaswara wanaosema kwamba Mwenyezi Mungu ni Al-Masīh mwana wa Maryam. Sema, ewe Mtume, kuwaambia Wanaswara hawa wajinga, «Lau Al-Masīh angalikuwa Mungu, kama wanavyodai, angaliweza kuuzuia uamuzi wa Mwenyezi Mungu ukimjia wa kumwangamiza yeye na mama yake na watu wote wa ardhini. Na mama yake ‘Īsā alikufa, hakuweza kumkinga na kifo. Vilevile hawezi kujitetea nafsi yake. Kwani wote wawili ni waja miongoni mwa waja wa Mwenyezi Mungu, hawawezi kujiepusha na maangamivu. Hii ni dalili kuwa yeye ni mwanadamu kama wanadamu wengine. Na vitu vyote vilivyoko mbinguni na ardhini ni milki ya Mwenyezi Mungu, Anaumba na kupatisha anachotaka na yeye ni muweza wa kila kitu. Hakika ya tawhīd (kumpwekesha Mwenyezi Mungu) inawajibisha kupwekeka Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, kwa sifa za uola na uungu; hakuna yoyote anayeshirikiana naye, katika viumbe Wake, kwa hilo. Na mara nyingi sana watu huingia kwenye ushirikina na upotevu kwa kuwatukuza Mitume na watu wema kupita kiasi, kama walivyopita kiasi Wanaswara katika kumtukuza Al-Masīh. Ulimwengu wote ni wa Mwenyezi Mungu, na viumbe viko kwenye mkono Wake Peke Yake. Na miujiza na alama kubwa zinazodhihiri, marejeo yake ni Mwenyezi Mungu.Anaumba, kutakasika na sifa za upungufu ni Kwake, na Anafanya Anachotaka. info
التفاسير: