《古兰经》译解 - 斯瓦希里语翻译 - 阿布杜拉·穆罕默德和纳赛尔·海米斯。

页码:close

external-link copy
17 : 40

ٱلۡيَوۡمَ تُجۡزَىٰ كُلُّ نَفۡسِۭ بِمَا كَسَبَتۡۚ لَا ظُلۡمَ ٱلۡيَوۡمَۚ إِنَّ ٱللَّهَ سَرِيعُ ٱلۡحِسَابِ

Leo italipwa kila nafsi kwa kile ilichokitenda duniani, chema au kiovu; hakuna maonevu leo kufanyiwa yoyote, ya kuongezewa dhambi zake au kupunguziwa thawabu zake. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwpesi wa kuhesabu, basi msiione Siku hiyo ni yenye kuchelewa kufika, kwani iko karibu. info
التفاسير:

external-link copy
18 : 40

وَأَنذِرۡهُمۡ يَوۡمَ ٱلۡأٓزِفَةِ إِذِ ٱلۡقُلُوبُ لَدَى ٱلۡحَنَاجِرِ كَٰظِمِينَۚ مَا لِلظَّٰلِمِينَ مِنۡ حَمِيمٖ وَلَا شَفِيعٖ يُطَاعُ

Na uwaonye watu, ewe Mtume, na Siku ya Kiyama iliyo karibu, ingawa wao waiona kuwa iko mbali, pindi nyoyo za waja, kwa kuogopa mateso ya Mwenyezi Mungu, zitakapopanda juu vifuani mwao na kushikana na koo zao, na hali wao wamejawa na hamu na huzuni. Madhalimu hawatakuwa na jamaa wa karibu wala rafiki wala muombezi wa kuwaombea kwa Mola wao akawa ni mwenye kukubaliwa. info
التفاسير:

external-link copy
19 : 40

يَعۡلَمُ خَآئِنَةَ ٱلۡأَعۡيُنِ وَمَا تُخۡفِي ٱلصُّدُورُ

Mwenyezi Mungu, Aliyetakasika na kila sifa ya upungufu, Anakijua kile kinachopitishwa na maangalizi ya macho kwa njia ya siri na kuiba na kile ambacho mtu anakidhamiria katika nafsi yake kizuri au kibaya. info
التفاسير:

external-link copy
20 : 40

وَٱللَّهُ يَقۡضِي بِٱلۡحَقِّۖ وَٱلَّذِينَ يَدۡعُونَ مِن دُونِهِۦ لَا يَقۡضُونَ بِشَيۡءٍۗ إِنَّ ٱللَّهَ هُوَ ٱلسَّمِيعُ ٱلۡبَصِيرُ

Na Mwenyezi Mungu Anahukumu baina ya watu kwa uadilifu kwa kumpa kila mtu haki yake. Na wale waungu wanaoabudiwa badala ya Mwenyezi Mungu, hawahukumu chochote kwa kutoweza kwao kufanya hivyo. Hakika Mwenyezi Mungu Ndiye Mwenye kuyasikia maneno ya waja Wake, Ndiye Mwenye kuyaona matendo wanayoyafanya, na Atawalipa kwayo. info
التفاسير:

external-link copy
21 : 40

۞ أَوَلَمۡ يَسِيرُواْ فِي ٱلۡأَرۡضِ فَيَنظُرُواْ كَيۡفَ كَانَ عَٰقِبَةُ ٱلَّذِينَ كَانُواْ مِن قَبۡلِهِمۡۚ كَانُواْ هُمۡ أَشَدَّ مِنۡهُمۡ قُوَّةٗ وَءَاثَارٗا فِي ٱلۡأَرۡضِ فَأَخَذَهُمُ ٱللَّهُ بِذُنُوبِهِمۡ وَمَا كَانَ لَهُم مِّنَ ٱللَّهِ مِن وَاقٖ

Kwani hawakutembea katika ardhi hawa wanaoukanusha utume wako, ewe Mtume, wakaangalia ulikuwa vipi mwisho wa ummah waliopita kabla yao? Walikuwa na nguvu zaidi kuliko wao na wenye athari zilizosalia muda mrefu zaidi, na hazikuwafaa wao nguvu zao nyingi wala miili yao mikubwa yenye nguvu, kwani Mwenyezi Mungu Aliwapatiliza kwa kuwatesa, kwa sababu ya ukafiri wao na kutenda kwao madhambi, na hawakuwa na mwokoaji wa kuwaokoa na adhabu ya Mwenyezi Mungu na kuizuia isiwafike. info
التفاسير:

external-link copy
22 : 40

ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمۡ كَانَت تَّأۡتِيهِمۡ رُسُلُهُم بِٱلۡبَيِّنَٰتِ فَكَفَرُواْ فَأَخَذَهُمُ ٱللَّهُۚ إِنَّهُۥ قَوِيّٞ شَدِيدُ ٱلۡعِقَابِ

Adhabu hiyo iliyowafikia wakanushaji waliopita ilikuwa ni kwa sababu ya msimamo wao juu ya Mitume ya Mwenyezi Mungu waliokuja na dalili za yakini za kuonesha ukweli wa madai yao, basi wakawakanusha na wakawafanya warongo na Mwenyezi Mungu Akawapatiliza kwa mateso Yake, hakika Yeye ni Mwenye nguvu hashindwi na yoyote, ni Mkali wa kutesa kwa aliyemkanusha na kumuasi. info
التفاسير:

external-link copy
23 : 40

وَلَقَدۡ أَرۡسَلۡنَا مُوسَىٰ بِـَٔايَٰتِنَا وَسُلۡطَٰنٖ مُّبِينٍ

Hakika tulimpelekea Mūsā alama zetu kubwa zenye kutolea ushahidi uhakika wa utume aliopewa na hoja zilizofunuka waziwazi juu ya ukweli wake katika ulinganizi wake, na kutanguka yale ambayo walikuwa nayo wale waliopelekewa hao Mitume. info
التفاسير:

external-link copy
24 : 40

إِلَىٰ فِرۡعَوۡنَ وَهَٰمَٰنَ وَقَٰرُونَ فَقَالُواْ سَٰحِرٞ كَذَّابٞ

Apate kuenda kwa Fir'awn, mfalme wa Misri, na Hāmān waziri wake, na Qārūn mwenye mali mengi na mahazina ya vitu vya thamani, wakaukanusha utume wake na wakafanya kiburi na wakamwambia, «Yeye ni mchawi mrongo sana, basi ni vipi anadai kuwa yeye ametumilizwa kwa watu kuwa ni Mtume?» info
التفاسير:

external-link copy
25 : 40

فَلَمَّا جَآءَهُم بِٱلۡحَقِّ مِنۡ عِندِنَا قَالُواْ ٱقۡتُلُوٓاْ أَبۡنَآءَ ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ مَعَهُۥ وَٱسۡتَحۡيُواْ نِسَآءَهُمۡۚ وَمَا كَيۡدُ ٱلۡكَٰفِرِينَ إِلَّا فِي ضَلَٰلٖ

Basi Mūsā alipomjia Fir'awn, Hāmān na Qārūn kwa miujiza iliyo waziwazi kutoka kwetu, hawakutosheka kwa kuipinga na kuikanusha , bali walisema, «waueni wana wa kiume wa wale walioamini pamoja naye na waacheni wanawake wao watumike na wafanywe watumwa. Na haikuwa mipango ya makafiri isipokuwa ni yenye kupita na kuangamia. info
التفاسير: