《古兰经》译解 - 斯瓦希里语翻译 - 阿布杜拉·穆罕默德和纳赛尔·海米斯。

external-link copy
21 : 33

لَّقَدۡ كَانَ لَكُمۡ فِي رَسُولِ ٱللَّهِ أُسۡوَةٌ حَسَنَةٞ لِّمَن كَانَ يَرۡجُواْ ٱللَّهَ وَٱلۡيَوۡمَ ٱلۡأٓخِرَ وَذَكَرَ ٱللَّهَ كَثِيرٗا

Hakika yenu nyinyi, enyi Waumini, mna mfano mwema wa kuiga katika maneno ya Mtume wa Mwenyezi Mungu, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, matendo yake na mwenendo wake. Basi jilazimisheni na mwenendo wake, kwani anaoufuata na kuuiga ni yule anayemtaraji Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho, Akamtaja Mwenyezi Mungu na kumuomba msamaha kwa wingi na akamshukuru kwa kila namna. info
التفاسير: