《古兰经》译解 - 斯瓦希里语翻译 - 阿布杜拉·穆罕默德和纳赛尔·海米斯。

external-link copy
176 : 3

وَلَا يَحۡزُنكَ ٱلَّذِينَ يُسَٰرِعُونَ فِي ٱلۡكُفۡرِۚ إِنَّهُمۡ لَن يَضُرُّواْ ٱللَّهَ شَيۡـٔٗاۚ يُرِيدُ ٱللَّهُ أَلَّا يَجۡعَلَ لَهُمۡ حَظّٗا فِي ٱلۡأٓخِرَةِۖ وَلَهُمۡ عَذَابٌ عَظِيمٌ

Wasikutie huzuni moyoni mwako hawa makafiri, ewe Mtume, kwa kukimbilia kwao kukanusha na kuingia kwenye upotevu. Hakika wao, kwa hilo, hawatamdhuru Mwenyezi Mungu chochote. Hakika ni kwamba wao wazidhuru nafsi zao kwa kuzinyima utamu wa Imani na thawabu kubwa. Mwenyezi Mungu Anataka Asiwape malipo mema yoyote huko Akhera, kwa kuwa wao wamejiepusha na ulinganizi wa haki. Na wao watapata adhabu kali. info
التفاسير: