《古兰经》译解 - 斯瓦希里语翻译 - 阿布杜拉·穆罕默德和纳赛尔·海米斯。

external-link copy
174 : 3

فَٱنقَلَبُواْ بِنِعۡمَةٖ مِّنَ ٱللَّهِ وَفَضۡلٖ لَّمۡ يَمۡسَسۡهُمۡ سُوٓءٞ وَٱتَّبَعُواْ رِضۡوَٰنَ ٱللَّهِۗ وَٱللَّهُ ذُو فَضۡلٍ عَظِيمٍ

Basi wakarudi kutoka Ḥamrā’ al Asad kuja Madina wakiwa wana neema za Mwenyezi Mungu kwa kupata thawabu nyingi na nyongeza za daraja ya juu zitokazo Kwake, huku Imani na yakini zimeongezeka kwao, maadui wa Mwenyezi Mungu wamewadhalilisha, wamefaulu kwa kusalimika na kuuawa na kupigana, na wamefuata mambo ya kumridhisha Mwenyezi Mungu kwa kumtii Yeye na Mtume Wake. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye ihsani na vipawa vingi vyenye kuwaenea wao na wengineo. info
التفاسير: