《古兰经》译解 - 斯瓦希里语翻译 - 阿布杜拉·穆罕默德和纳赛尔·海米斯。

external-link copy
159 : 3

فَبِمَا رَحۡمَةٖ مِّنَ ٱللَّهِ لِنتَ لَهُمۡۖ وَلَوۡ كُنتَ فَظًّا غَلِيظَ ٱلۡقَلۡبِ لَٱنفَضُّواْ مِنۡ حَوۡلِكَۖ فَٱعۡفُ عَنۡهُمۡ وَٱسۡتَغۡفِرۡ لَهُمۡ وَشَاوِرۡهُمۡ فِي ٱلۡأَمۡرِۖ فَإِذَا عَزَمۡتَ فَتَوَكَّلۡ عَلَى ٱللَّهِۚ إِنَّ ٱللَّهَ يُحِبُّ ٱلۡمُتَوَكِّلِينَ

Na kwa ajili ya rehema za Mwenyezi Mungu kwako na maswhaba wako, ewe Nabii, Mwenyezi Mungu Alikuneemesha ukawa laini kwao. Na lau ungalikuwa na tabia mbaya, mwenye moyo mgumu, maswahaba wako wangalijitenga na kuwa mbali na wewe. Kwa hivyo, usiwe na hasira nao kwa yaliyotokea kwao katika vita vya Uhud. Basi muombe Mwenyezi Mungu, ewe Nabii, Awasamehe na uwashauri katika mambo yanayohitajia ushauri. Na utakapoazimia kufanya jambo kati ya mambo yoyote, baada ya kushauri, litekeleze hali ya kumtegemea Mwenyezi Mungu, Peke Yake. Hakika Mwenyezi Mungu Anawapenda wenye kujitegemeza Kwake. info
التفاسير: