《古兰经》译解 - 斯瓦希里语翻译 - 阿布杜拉·穆罕默德和纳赛尔·海米斯。

external-link copy
79 : 17

وَمِنَ ٱلَّيۡلِ فَتَهَجَّدۡ بِهِۦ نَافِلَةٗ لَّكَ عَسَىٰٓ أَن يَبۡعَثَكَ رَبُّكَ مَقَامٗا مَّحۡمُودٗا

Na inuka, ewe Nabii, kutoka kwenye usingizi sehemu ya usiku, usome Qur’ani katika Swala ya usiku, ipate kuwa, hiyo Swala ya usiku, ni nyongeza kwako katika utukufu wa cheo na kupandishiwa daraja. Huenda Mwenyezi Mungu Akakuleta uwe ni mwenye kuwashufaia watu Siku ya Kiyama, ili Mwenyezi Mungu Awarehemu kwa kuwaondolea waliokuwa nayo, na usimame kisimamo ambacho watakushukuru kwacho wa mwanzo na wa mwisho. info
التفاسير: