《古兰经》译解 - 斯瓦希里语翻译 - 阿布杜拉·穆罕默德和纳赛尔·海米斯。

external-link copy
70 : 16

وَٱللَّهُ خَلَقَكُمۡ ثُمَّ يَتَوَفَّىٰكُمۡۚ وَمِنكُم مَّن يُرَدُّ إِلَىٰٓ أَرۡذَلِ ٱلۡعُمُرِ لِكَيۡ لَا يَعۡلَمَ بَعۡدَ عِلۡمٖ شَيۡـًٔاۚ إِنَّ ٱللَّهَ عَلِيمٞ قَدِيرٞ

Na mwenyezi Mungu, kutakata na sifa za upungufu ni Kwake na kutukuka ni Kwake, Amewaumba, kisha Atawafisha katika mwisho wa umri wenu. Na kati yenu kuna wale ambao watafikia umri muovu, nao ni ukongwe, kama alivyokuwa uchangani mwake, hajui chochote ambacho alikuwa akikijua. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mjuzi, ni muweza, ujuzi Wake na uweza wake vimezunguka kila kitu. Mwenyezi Mungu Aliyemrudisha mwanadamu kwenye hali hii ni muweza wa kumfisha kisha kumfufua. info
التفاسير: