《古兰经》译解 - 斯瓦希里语翻译 - 阿布杜拉·穆罕默德和纳赛尔·海米斯。

external-link copy
28 : 10

وَيَوۡمَ نَحۡشُرُهُمۡ جَمِيعٗا ثُمَّ نَقُولُ لِلَّذِينَ أَشۡرَكُواْ مَكَانَكُمۡ أَنتُمۡ وَشُرَكَآؤُكُمۡۚ فَزَيَّلۡنَا بَيۡنَهُمۡۖ وَقَالَ شُرَكَآؤُهُم مَّا كُنتُمۡ إِيَّانَا تَعۡبُدُونَ

Kumbuka, ewe Mtume, Siku ambayo tutawafufua viumbe wote ili wahesabiwe na walipwe, kisha tuseme kuwaambia waliomshirikisha Mwenyezi Mungu, «Jilazimisheni mahali mliopo, nyinyi na washirika wenu ambao mlikuwa mkiwaabudu badala ya Mwenyezi Mungu, mpaka tuangalie mtafanya nini.» Hapo tutapambanua baina ya washirikina na wale wanaowaabudu, na watajitenga, wale walioabudiwa badala ya Mwenyezi Mungu, na wale waliokuwa wanawaabudu, na watasema kuwaambia washirikina «Hamkuwa mkituabudu sisi ulimwenguni.» info
التفاسير: