Salin ng mga Kahulugan ng Marangal na Qur'an - Salin sa Wikang Swahili ni Ali Mohsin Al-Barwani

Al-Qadr

external-link copy
1 : 97

إِنَّآ أَنزَلۡنَٰهُ فِي لَيۡلَةِ ٱلۡقَدۡرِ

Hakika Sisi tumeiteremsha Qur'ani katika Laylatul Qadri, Usiku wa Cheo Kitukufu. [1] info

[1] Hakika Sisi tumeiteremsha Qur'ani katika usiku wa Cheo na Utukufu.

التفاسير:

external-link copy
2 : 97

وَمَآ أَدۡرَىٰكَ مَا لَيۡلَةُ ٱلۡقَدۡرِ

Na nini kitacho kujuulisha nini Laylatul Qadri? [2] info

[2] Na kitu gani kitakufunza ni nini usiku huo wa Cheo na Utukufu?

التفاسير:

external-link copy
3 : 97

لَيۡلَةُ ٱلۡقَدۡرِ خَيۡرٞ مِّنۡ أَلۡفِ شَهۡرٖ

Laylatul Qadri ni bora kuliko miezi elfu. [3] info

[3] Usiku wa Qadr na Sharaf, Cheo na Utukufu, ni bora kuliko miezi elfu, kwa kuwa umekhusika kwa kuteremka ndani yake Qur'ani tukufu.

التفاسير:

external-link copy
4 : 97

تَنَزَّلُ ٱلۡمَلَٰٓئِكَةُ وَٱلرُّوحُ فِيهَا بِإِذۡنِ رَبِّهِم مِّن كُلِّ أَمۡرٖ

Huteremka Malaika na Roho katika usiku huo kwa idhini ya Mola wao Mlezi kwa kila jambo. [4] info

[4] Huteremka Malaika na Jibrili katika usiku huo mpaka kwenye ardhi kwa idhini ya Mola wao Mlezi kwa sababu ya kila jambo.

التفاسير:

external-link copy
5 : 97

سَلَٰمٌ هِيَ حَتَّىٰ مَطۡلَعِ ٱلۡفَجۡرِ

Amani usiku huo mpaka mapambazuko ya alfajiri. [5] info

[5] Na wameaminika na maudhi na uovu. Hali inabaki hivyo mpaka mapambazuko ya alfajiri.

التفاسير: