Na ikamwelekea Mola wake Mlezi kwa kuzidi kutanuka kwake na kutoa vilio kuwemo ndani yake na kuachana navyo, na hayo ni haki yake kuwa. Yakitokea yote hayo yaliyo tangulia kusimuliwa basi kila mtu atapata malipo ya vitendo vyake.
Ewe mtu! Hakika wewe unafanya juhudi katika vitendo vyako vikufikishie lengo lako. Basi utakuja kukutana na Mola wako Mlezi kwa a'mali yako, naye atakulipa kwayo.
Lakini walio amini na wakatenda mema watapata, kutoka kwa Mwenyezi Mungu, ujira usio wakatikia na wala usio kuwa na hisabu juu yao.