Salin ng mga Kahulugan ng Marangal na Qur'an - Salin sa Wikang Swahili nina Abdullah Muhammad at Nasir Khamis

external-link copy
49 : 7

أَهَٰٓؤُلَآءِ ٱلَّذِينَ أَقۡسَمۡتُمۡ لَا يَنَالُهُمُ ٱللَّهُ بِرَحۡمَةٍۚ ٱدۡخُلُواْ ٱلۡجَنَّةَ لَا خَوۡفٌ عَلَيۡكُمۡ وَلَآ أَنتُمۡ تَحۡزَنُونَ

Je madhaifu na mafukara hawa, kati ya watu wa Peponi, ndio wale mlioapa huko duniani kwamba Mwenyezi Mungu Hatawakusanya Siku ya Kiyama Awatie kwenye rehema na Hatawaingiza Peponi? Ingieni Peponi, enyi watu wa Al- A'rāf, hakika mumesamehewa; hamna tene kicho cha kupata adhabu ya Mwenyezi Mungu, wala hamtahuzunika juu ya hadhi za duniani zilizowapita. info
التفاسير: