Salin ng mga Kahulugan ng Marangal na Qur'an - Salin sa Wikang Swahili nina Abdullah Muhammad at Nasir Khamis

Numero ng Pahina:close

external-link copy
164 : 7

وَإِذۡ قَالَتۡ أُمَّةٞ مِّنۡهُمۡ لِمَ تَعِظُونَ قَوۡمًا ٱللَّهُ مُهۡلِكُهُمۡ أَوۡ مُعَذِّبُهُمۡ عَذَابٗا شَدِيدٗاۖ قَالُواْ مَعۡذِرَةً إِلَىٰ رَبِّكُمۡ وَلَعَلَّهُمۡ يَتَّقُونَ

Na kumbuka, ewe Mtume, pindi kundi kati yao waliposema kuwaambia kundi lingine lililokuwa likiwapa mawaidhia wale waliopita mipaka siku ya Jumamosi na likiwakataza wasimuasi Mwenyezi Mungu siku hiyo, «Kwa nini nyinyi mnawaidhia watu ambao Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuwaangamiza ulimwenguni kwa kumuasi au ni Mwenye kuwaadhibu adhabu kali kesho Akhera?» Wakanena wale waliokuwa wakiwakataza wasimuasi Mwenyezi Mungu, «Tunawaidhia na tunawakataza ili tuwe na udhuru kuhusu wao na kwa ajili ya kutekeleza wajibu wa Mwenyezi Mungu juu yetu ya kuamrisha mema na kukataza maovu na kwa matumaini kwamba watamcha Mwenyezi Mungu, watamuogopa na watatubia kutokana na kumuasi kwao Mola wao na kupita mipaka ya mambo yaliyoharamishiwa kwao.» info
التفاسير:

external-link copy
165 : 7

فَلَمَّا نَسُواْ مَا ذُكِّرُواْ بِهِۦٓ أَنجَيۡنَا ٱلَّذِينَ يَنۡهَوۡنَ عَنِ ٱلسُّوٓءِ وَأَخَذۡنَا ٱلَّذِينَ ظَلَمُواْ بِعَذَابِۭ بَـِٔيسِۭ بِمَا كَانُواْ يَفۡسُقُونَ

Basi lilipoacha lile pote ambalo lilikiuka mipaka siku ya Jumamosi yale waliyokumbushwa na likaendelea kwenye upotevu wake na kukiuka mipaka kwake katika siku hiyo na lisiyakubali mawaidha waliyopewa na pote lenye kuwaidhia, Mwenyezi Mungu Aliwaokoa wale waliokuwa wanakataza maasia Yake na akawapatia wale waliokiuka mipaka siku ya Jumamosi adhabu kali mno kwa sababu ya kuenda kinyume kwao na amri ya Mwenyezi Mungu na kutoka kwao kwenye utiifu Wake. info
التفاسير:

external-link copy
166 : 7

فَلَمَّا عَتَوۡاْ عَن مَّا نُهُواْ عَنۡهُ قُلۡنَا لَهُمۡ كُونُواْ قِرَدَةً خَٰسِـِٔينَ

Basi pote hilo lilipoasi na likayakiuka yale ambayo Mwenyezi Mungu Alioyakataza ya kutowinda siku ya siku ya Jumamosi, Mwenyezi Mungu Aliwaambia (watu wa pote hilo), «Kuweni manyani hali ni wanyoge ni wenye kuwekwa mbali na kila jema.» Na wakawa hivyo. info
التفاسير:

external-link copy
167 : 7

وَإِذۡ تَأَذَّنَ رَبُّكَ لَيَبۡعَثَنَّ عَلَيۡهِمۡ إِلَىٰ يَوۡمِ ٱلۡقِيَٰمَةِ مَن يَسُومُهُمۡ سُوٓءَ ٱلۡعَذَابِۗ إِنَّ رَبَّكَ لَسَرِيعُ ٱلۡعِقَابِ وَإِنَّهُۥ لَغَفُورٞ رَّحِيمٞ

Na kumbuka, ewe Mtume, pindi Alipotangaza Mola wako, tangazo wazi, kwamba Atawapelekea Mayahudi mwenye kuwaonjesha adhabu mbaya na kuwadhalilisha mpaka Siku ya Kiyama. Hakika Mola wako ni Mpesi wa kutesa kwa anayestahili kuteswa kwa sababu ya ukafiri wake na uasi wake. Na hakika Yeye ni Mwingi wa kusamehe dhambi za wenye kutubia, ni Mwnye huruma kwao. info
التفاسير:

external-link copy
168 : 7

وَقَطَّعۡنَٰهُمۡ فِي ٱلۡأَرۡضِ أُمَمٗاۖ مِّنۡهُمُ ٱلصَّٰلِحُونَ وَمِنۡهُمۡ دُونَ ذَٰلِكَۖ وَبَلَوۡنَٰهُم بِٱلۡحَسَنَٰتِ وَٱلسَّيِّـَٔاتِ لَعَلَّهُمۡ يَرۡجِعُونَ

Na tuliwagawanya Wana wa Isrāīl makundi: kati yao kuna wanaosimama kutekeleza haki za Mwenyezi Mungu na haki za waja Wake, na kati yao kuna wenye kufanya kasoro wenye kuzidhulumu nafsi zao. Na hawa tuliwapa mtihani wa maisha ya neema na ukunjufu wa riziki; na pia tuliwapa mtihani wa maisha ya dhiki, misiba na matatizo kwa matarajio kuwa watarudi kumtii Mola wao na watatubia kutokana na vitendo vya kumuasi. info
التفاسير:

external-link copy
169 : 7

فَخَلَفَ مِنۢ بَعۡدِهِمۡ خَلۡفٞ وَرِثُواْ ٱلۡكِتَٰبَ يَأۡخُذُونَ عَرَضَ هَٰذَا ٱلۡأَدۡنَىٰ وَيَقُولُونَ سَيُغۡفَرُ لَنَا وَإِن يَأۡتِهِمۡ عَرَضٞ مِّثۡلُهُۥ يَأۡخُذُوهُۚ أَلَمۡ يُؤۡخَذۡ عَلَيۡهِم مِّيثَٰقُ ٱلۡكِتَٰبِ أَن لَّا يَقُولُواْ عَلَى ٱللَّهِ إِلَّا ٱلۡحَقَّ وَدَرَسُواْ مَا فِيهِۗ وَٱلدَّارُ ٱلۡأٓخِرَةُ خَيۡرٞ لِّلَّذِينَ يَتَّقُونَۚ أَفَلَا تَعۡقِلُونَ

Wakaja, baada ya hawa ambao tulieleza sifa zao, badala mbovu. Walichukua Kitabu kutoka kwa wakale wao, wakakisoma na wakakijua, na wakaenda kinyume na hukumu zake, wakawa wanachukua kile wanacholetewa cha starahe ya ulimwenguni kinachotokana na njia mbaya za mapato kama hongo na mfano wake. Hayo ni kwa sababu ya wingi wa pupa lao na uroho wao, na wanasema pamoja na hayo, «Mwenyezi Mungu Atatusamehe,» wakitamani kwa Mwenyezi Mungu mambo yasiyofaa, na ikiwajia Mayahudi hawa starahe yenye kuondoka, miongoni mwa vitu vya haramu, huichukua na kuihalalisha, huku wakiendelea kufanya madhambi yao na kutumia haramu. Kwani hazikuchukuliwa kwao ahadi juu ya kuisimamisha Taurati na kufuata kivitendo yaliyomo ndani yake na kwamba hawatasema juu ya Mwenyezi Mungu isipokuwa ukweli na kwamba hawatamzulia urongo, wakayajua yaliyomo Kitabuni, wakayapoteza na wakaenda kinyume na ahadi ya Mwenyezi Mungu kwao katika hilo? Na nyumba ya Akhera ni bora zaidi kwa wanaomcha Mwenyezi Mungu, wakafuata amri Zake na wakaepuka makatazo Yake. Kwani hawa wanaochukua mapato duni hawaelewi kwamba yaliyo mbele ya Mwenyezi Mungu ni bora zaidi na yenye kusalia zaidi kwa wachamungu? info
التفاسير:

external-link copy
170 : 7

وَٱلَّذِينَ يُمَسِّكُونَ بِٱلۡكِتَٰبِ وَأَقَامُواْ ٱلصَّلَوٰةَ إِنَّا لَا نُضِيعُ أَجۡرَ ٱلۡمُصۡلِحِينَ

Na wanaoshikamana na Kitabu, wanaoyafuata kivitendo yaliyomo ndani yake miongoni mwa mambo ya itikadi na hukumu na wanaodumu na Swala kwa mipaka yake na wasiyozipoteza nyakati zake, Mwenyezi Mungu Atawalipa kwa matendo yao mema na hatayapoteza. info
التفاسير: