Salin ng mga Kahulugan ng Marangal na Qur'an - Salin sa Wikang Swahili nina Abdullah Muhammad at Nasir Khamis

external-link copy
99 : 5

مَّا عَلَى ٱلرَّسُولِ إِلَّا ٱلۡبَلَٰغُۗ وَٱللَّهُ يَعۡلَمُ مَا تُبۡدُونَ وَمَا تَكۡتُمُونَ

Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, Anawaelezea kwamba shughuli ya Mtume Wake , rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, ni kuongoza kwa kuelekeza na kufikisha na kwamba uongofu wa taufiki uko mkononi mwa Mwenyezi Mungu, Peke Yake, na kwamba mambo yaliyomo ndani ya nafsi za watu, katika yale wanayoyafanya kwa siri na wanayoyatangaza, ya uongofu na upotevu, Mwenyezi Mungu Anayajua.. info
التفاسير: