Salin ng mga Kahulugan ng Marangal na Qur'an - Salin sa Wikang Swahili nina Abdullah Muhammad at Nasir Khamis

external-link copy
59 : 5

قُلۡ يَٰٓأَهۡلَ ٱلۡكِتَٰبِ هَلۡ تَنقِمُونَ مِنَّآ إِلَّآ أَنۡ ءَامَنَّا بِٱللَّهِ وَمَآ أُنزِلَ إِلَيۡنَا وَمَآ أُنزِلَ مِن قَبۡلُ وَأَنَّ أَكۡثَرَكُمۡ فَٰسِقُونَ

Sema, ewe Mtume, kuwaambia hao wanaofanya shere kati ya hao waliiopewa Kitabu, «Mnalolikuta kuwa ni jambo la kutukanika au ni la aibu, hilo kwetu ni zuri kusifika nalo. Na hilo ni lile la kumuamini kwetu Mwenyezi Mungu na vitabu Vyake vilivyoteremshwa kwetu na waliokuwa kabla yetu na kuamini kwetu kwamba wengi wenu muko nje ya njia ilyo nyofu.» info
التفاسير: