Salin ng mga Kahulugan ng Marangal na Qur'an - Salin sa Wikang Swahili nina Abdullah Muhammad at Nasir Khamis

external-link copy
15 : 5

يَٰٓأَهۡلَ ٱلۡكِتَٰبِ قَدۡ جَآءَكُمۡ رَسُولُنَا يُبَيِّنُ لَكُمۡ كَثِيرٗا مِّمَّا كُنتُمۡ تُخۡفُونَ مِنَ ٱلۡكِتَٰبِ وَيَعۡفُواْ عَن كَثِيرٖۚ قَدۡ جَآءَكُم مِّنَ ٱللَّهِ نُورٞ وَكِتَٰبٞ مُّبِينٞ

Enyi watu mliopewa Kitabu , miongoni mwa Mayahudi na Wanaswara! Amewajia nyinyi mjumbe wetu Muhammad , rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, kuwafafanulia mengi ambayo mlikuwa mkiyaficha kwa watu katika yale yaliyomo ndani ya Taurati na Injili, na kuacha kuyafafanua yale ambayo busara haitaki yafafanuliwe. Hakika umewajia kutoka kwa Mwenyezi Mungu mwngaza na Kitabu chenye ufafanuzi, nacho ni Qur’ani tukufu. info
التفاسير: