Salin ng mga Kahulugan ng Marangal na Qur'an - Salin sa Wikang Swahili nina Abdullah Muhammad at Nasir Khamis

external-link copy
178 : 3

وَلَا يَحۡسَبَنَّ ٱلَّذِينَ كَفَرُوٓاْ أَنَّمَا نُمۡلِي لَهُمۡ خَيۡرٞ لِّأَنفُسِهِمۡۚ إِنَّمَا نُمۡلِي لَهُمۡ لِيَزۡدَادُوٓاْ إِثۡمٗاۖ وَلَهُمۡ عَذَابٞ مُّهِينٞ

Wala wasidhani wakanushaji kwamba sisi tukiwarefushia umri wao, tukawastarehesha kwa starehe za duniani na tusiwaadhibu kwa ukafiri wao na madhambi yao kwamba watakuwa wamepata heri ya nafsi zao. Hakika tunawacheleweshea adhabu na ajali zao ili wazidishe dhuluma na ukeukaji mipaka. Na watapata adhabu yenye kuwadhalilisha na kuwatweza. info
التفاسير: