Salin ng mga Kahulugan ng Marangal na Qur'an - Salin sa Wikang Swahili nina Abdullah Muhammad at Nasir Khamis

external-link copy
46 : 22

أَفَلَمۡ يَسِيرُواْ فِي ٱلۡأَرۡضِ فَتَكُونَ لَهُمۡ قُلُوبٞ يَعۡقِلُونَ بِهَآ أَوۡ ءَاذَانٞ يَسۡمَعُونَ بِهَاۖ فَإِنَّهَا لَا تَعۡمَى ٱلۡأَبۡصَٰرُ وَلَٰكِن تَعۡمَى ٱلۡقُلُوبُ ٱلَّتِي فِي ٱلصُّدُورِ

Si watembee hao wakanushaji wa Makureshi kwenye ardhi wajionee athari za walioangamizwa, wafikirie kwa akili zao na wazingatie na wasikie habari zao kusikia kwa mazingatio wapate kuwaidhika? Kwani upofu si upofu wa macho, hakika ya upofu wenye kuangamiza ni upofu wa busara wa kutoijua haki na kutozingatia. info
التفاسير: