Salin ng mga Kahulugan ng Marangal na Qur'an - Salin sa Wikang Swahili nina Abdullah Muhammad at Nasir Khamis

external-link copy
39 : 22

أُذِنَ لِلَّذِينَ يُقَٰتَلُونَ بِأَنَّهُمۡ ظُلِمُواْۚ وَإِنَّ ٱللَّهَ عَلَىٰ نَصۡرِهِمۡ لَقَدِيرٌ

Waislamu, mwanzo wao, walikuwa wamekatazwa kupigana na makafiri, wameamrishwa kuvumilia maudhi yao. Maudhi ya washirikina yalipofikia upeo wake na Mtume akatoka Makkah hali ya kugura kwenda Madina na Uislamu ukawa na nguvu, Mwenyezi Mungu Aliwaruhusu Waislamu kupigana kwa sababu hiyo ya maonevu yaliyowashukia na uadui. Na Mwenyezi Mungu ni Muweza wa kuwanusuru na kuwadhalilisha maadui wao. info
التفاسير: