Salin ng mga Kahulugan ng Marangal na Qur'an - Salin sa Wikang Swahili nina Abdullah Muhammad at Nasir Khamis

external-link copy
25 : 17

رَّبُّكُمۡ أَعۡلَمُ بِمَا فِي نُفُوسِكُمۡۚ إِن تَكُونُواْ صَٰلِحِينَ فَإِنَّهُۥ كَانَ لِلۡأَوَّٰبِينَ غَفُورٗا

Mola wenu, enyi watu, ni Mjuzi zaidi wa mazuri na mabaya yaliyomo ndani ya nyoyo zenu. Iwapo matakwa yenu na makusudio yenu ni kumridhisha Mwenyezi Mungu na kujikaribisha Kwake, basi Yeye, kutakata na sifa mbaya ni Kwake, kwa wenye kurejea Kwake katika nyakati zote ni Mwingi wa kusamehe. Basi yoyote yule ambaye Mwenyezi Mungu Amejua kwamba hakuna katika moyo wake isipokuwa ni kurejea Kwake na kumpenda, Yeye Atamsamehe na Atamghufiria yatakayotukia miongoni mwa madhambi madogo yanayolingana na tabia za kibinadamu. info
التفاسير: