Salin ng mga Kahulugan ng Marangal na Qur'an - Salin sa Wikang Swahili nina Abdullah Muhammad at Nasir Khamis

Ar-Ra'd

external-link copy
1 : 13

الٓمٓرۚ تِلۡكَ ءَايَٰتُ ٱلۡكِتَٰبِۗ وَٱلَّذِيٓ أُنزِلَ إِلَيۡكَ مِن رَّبِّكَ ٱلۡحَقُّ وَلَٰكِنَّ أَكۡثَرَ ٱلنَّاسِ لَا يُؤۡمِنُونَ

Alif, Lām, Mīm. Maelezo kuhusu herufi ziliokatwa na kutengwa yametangulia mwanzo wa sura ya Al-Baqarah. Hizi ni aya za Qur’ani zenye cheo kitukufu. Na Qur’ani hii uliyoteremshiwa, ewe Mtume, ndiyo haki, na sivyo kama vile wanavyosema washirikina kwamba wewe mwenyewe ndio uliyoileta. Pamoja na hili, wengi wa watu hawaiamini wala hawaifuati kivitendo. info
التفاسير:

external-link copy
2 : 13

ٱللَّهُ ٱلَّذِي رَفَعَ ٱلسَّمَٰوَٰتِ بِغَيۡرِ عَمَدٖ تَرَوۡنَهَاۖ ثُمَّ ٱسۡتَوَىٰ عَلَى ٱلۡعَرۡشِۖ وَسَخَّرَ ٱلشَّمۡسَ وَٱلۡقَمَرَۖ كُلّٞ يَجۡرِي لِأَجَلٖ مُّسَمّٗىۚ يُدَبِّرُ ٱلۡأَمۡرَ يُفَصِّلُ ٱلۡأٓيَٰتِ لَعَلَّكُم بِلِقَآءِ رَبِّكُمۡ تُوقِنُونَ

Mwenyezi Mungu Aliyetukuka Ndiye Aliyeziinua mbingu saba kwa uweza Wake bila ya nguzo, kama vile ambavyo mnaziona, kisha akalingana - yaani akawa juu - ya Arshi kulingana kunakonasibiana na utukufu Wake na ukubwa Wake, na Akalidhalilisha jua na mwezi kwa manufaa ya waja, kila moja wapo ya viwili hivyo kinazunguka kwenye anga lake mpaka Siku ya Kiyama. Anapekesha, kutakata na sifa za upungufu ni Kwake, mambo ya ulimwenguni na Akhera, Anawafafanulia dalili zenye kuonyesha uweza Wake na kwamba yeye hakuna mungu isipokuwa Yeye, ili muwe na Imani ya kikweli kwa Mwenyezi Mungu na mjiyakinishe kurudi Kwake, mpate kuamini ahadi Yake ya thawabu na adhabu na mumtakasiye ibada Peke Yake. info
التفاسير:

external-link copy
3 : 13

وَهُوَ ٱلَّذِي مَدَّ ٱلۡأَرۡضَ وَجَعَلَ فِيهَا رَوَٰسِيَ وَأَنۡهَٰرٗاۖ وَمِن كُلِّ ٱلثَّمَرَٰتِ جَعَلَ فِيهَا زَوۡجَيۡنِ ٱثۡنَيۡنِۖ يُغۡشِي ٱلَّيۡلَ ٱلنَّهَارَۚ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَأٓيَٰتٖ لِّقَوۡمٖ يَتَفَكَّرُونَ

Na Yeye, kutakata na sifa za upungufu ni Kwake, Ndiye Ambaye Aliifanya ardhi iwe kunjufu iliyonyoshwa, Akaitayarisha kwa maisha yenu, Akayaweka humo majabali yenye kuithibitisha na mito ya nyinyi kunywa na kunufaika, Akaweka humo aina mbili za kila matunda, katika hayo kukawa kuna meupe na meusi, tamu na kali, na Akaufanya usiku ufinike mchana kwa giza lake. Hakika katika hayo yote pana mazingatio kwa wenye kuyafikiri wakawaidhika. info
التفاسير:

external-link copy
4 : 13

وَفِي ٱلۡأَرۡضِ قِطَعٞ مُّتَجَٰوِرَٰتٞ وَجَنَّٰتٞ مِّنۡ أَعۡنَٰبٖ وَزَرۡعٞ وَنَخِيلٞ صِنۡوَانٞ وَغَيۡرُ صِنۡوَانٖ يُسۡقَىٰ بِمَآءٖ وَٰحِدٖ وَنُفَضِّلُ بَعۡضَهَا عَلَىٰ بَعۡضٖ فِي ٱلۡأُكُلِۚ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَأٓيَٰتٖ لِّقَوۡمٖ يَعۡقِلُونَ

Na kwenye ardhi kuna sehemu zinaopakana, kati ya hizo kuna zilizo nzuri zenye kuota mimea inayowafaa watu na kati ya hizo kuna kavu zenye chumvi zisizootesha chochote. Na katika ardhi nzuri kuna mashamba ya zabibu, na Amejaalia humo aina tafauti za makulima na mitende iliyokusanyika mahali pamoja na isiyokusanyika hapo, vyote hivyo viko katika mchanga mmoja na vinakunywa maji mamoja, isipokuwa vinatafautiana katika matunda, ukubwa, utamu na mengineyo: hili ni tamu na hili ni kali, na mengine ni bora kuliko mengine katika kula. Katika hilo kuna dalili kwa mwenye moyo unaoyaelewa maamrisho ya Mwenyezi Mungu na makatazo Yake. info
التفاسير:

external-link copy
5 : 13

۞ وَإِن تَعۡجَبۡ فَعَجَبٞ قَوۡلُهُمۡ أَءِذَا كُنَّا تُرَٰبًا أَءِنَّا لَفِي خَلۡقٖ جَدِيدٍۗ أُوْلَٰٓئِكَ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ بِرَبِّهِمۡۖ وَأُوْلَٰٓئِكَ ٱلۡأَغۡلَٰلُ فِيٓ أَعۡنَاقِهِمۡۖ وَأُوْلَٰٓئِكَ أَصۡحَٰبُ ٱلنَّارِۖ هُمۡ فِيهَا خَٰلِدُونَ

Ukiona ajabu , ewe Mtume, ya makafiri kutoamini baada ya dalili hizi, basi ajabu kubwa zaidi ni kusema kwao, «Je, tukifa na tukawa mchanga tutafufuliwa upya?» Hao ndio wenye kumkanusha Mola wao Aliyewafanya waweko kutoka kwenye hali ya kutokuwako. Na hao kutakuwa na minyororo kwenye shingo zao Siku ya Kiyama. Na hao wataingia Motoni na hawatatoka kabisa. info
التفاسير: