పవిత్ర ఖురాన్ యొక్క భావార్థాల అనువాదం - స్వాహిలి అనువాదం - అలీ ముహ్సిన్ అల్ బర్వానీ

At-Takwir

external-link copy
1 : 81

إِذَا ٱلشَّمۡسُ كُوِّرَتۡ

Jua litakapo kunjwa! info

Jua litakapo kunjwa na mwangaza wake ukafutwa,

التفاسير:

external-link copy
2 : 81

وَإِذَا ٱلنُّجُومُ ٱنكَدَرَتۡ

Na nyota zikazimwa! info

Na nyota ikazimwa nuru yao,

التفاسير:

external-link copy
3 : 81

وَإِذَا ٱلۡجِبَالُ سُيِّرَتۡ

Na milima ikaondolewa! info

Na milima ikaondoshwa hapo ilipo,

التفاسير:

external-link copy
4 : 81

وَإِذَا ٱلۡعِشَارُ عُطِّلَتۡ

Na ngamia wenye mimba pevu watakapo achwa wasishughulikiwe, info

Na ambao wa kuchukua mimba wakaharibu mimba zao,

التفاسير:

external-link copy
5 : 81

وَإِذَا ٱلۡوُحُوشُ حُشِرَتۡ

Na wanyama wa mwituni wakakusanywa! info

Na nyama mwitu wakusanywe kutoka vichakani mwao na mashimoni mwao, hawajijui hawajitambui kwa wingi wa kufazaika.

التفاسير:

external-link copy
6 : 81

وَإِذَا ٱلۡبِحَارُ سُجِّرَتۡ

Na bahari zikawaka moto! info

Na bahari zikawa zinawaka moto,

التفاسير:

external-link copy
7 : 81

وَإِذَا ٱلنُّفُوسُ زُوِّجَتۡ

Na nafsi zikaunganishwa! info

Na roho zikaunganishwa na viwiliwili vyao,

التفاسير:

external-link copy
8 : 81

وَإِذَا ٱلۡمَوۡءُۥدَةُ سُئِلَتۡ

Na msichana aliye zikwa hai atapo ulizwa! info

Na mtoto wa kike aliye zikwa hai, akaulizwa kwa kumliwaza yeye, na kumshutumu aliye mzika hai,

التفاسير:

external-link copy
9 : 81

بِأَيِّ ذَنۢبٖ قُتِلَتۡ

Kwa kosa gani aliuliwa? info

Kwa makosa gani kauliwa, naye hana dhambi? (Ilikuwa ada ya makafiri wa Kiarabu kabla ya Uislamu kuwazika watoto wao wa kike nao wahai! Baadhi ya Mabaniani wanawauwa watoto wao wa kike hata hivi leo huko India!!)

التفاسير:

external-link copy
10 : 81

وَإِذَا ٱلصُّحُفُ نُشِرَتۡ

Na madaftari yatakapo enezwa, info

Na nyaraka zilizo andikwa ndani vitendo vya watu zikakunjuliwa wakati wa hisabu.

التفاسير:

external-link copy
11 : 81

وَإِذَا ٱلسَّمَآءُ كُشِطَتۡ

 Na mbingu itapo tanduliwa, info

Na mbingu itapo ondoshwa pahala pake,

التفاسير:

external-link copy
12 : 81

وَإِذَا ٱلۡجَحِيمُ سُعِّرَتۡ

Na Jahannamu itapo chochewa, info

Na Moto ukawashwa kwa mwako mkali,

التفاسير:

external-link copy
13 : 81

وَإِذَا ٱلۡجَنَّةُ أُزۡلِفَتۡ

Na Pepo ikasogezwa, info

Na Pepo ikajongezwa ikawa karibu,

التفاسير:

external-link copy
14 : 81

عَلِمَتۡ نَفۡسٞ مَّآ أَحۡضَرَتۡ

Kila nafsi itajua ilicho kihudhurisha. info

Yatakapo tokea yote hayo, basi hapo tena kila nafsi itajua nini iliyo tanguliza, ikiwa kheri au shari.

التفاسير:

external-link copy
15 : 81

فَلَآ أُقۡسِمُ بِٱلۡخُنَّسِ

Naapa kwa nyota zinapo rejea nyuma, info

Naapa kiapo cha mkazo kwa nyota ambazo zinanywea zinapo chomoza, na hapo mwanga wake huwa khafifu,

التفاسير:

external-link copy
16 : 81

ٱلۡجَوَارِ ٱلۡكُنَّسِ

Zinazo kwenda, kisha zikajificha, info

Zenye kwenda na hujificha wakati wa kuchwa kwake, kama paa wanapo jificha kwenye mapango yao.

التفاسير:

external-link copy
17 : 81

وَٱلَّيۡلِ إِذَا عَسۡعَسَ

Na kwa usiku unapo pungua, info

Na kwa usiku linapo pungua giza lake wakati unapo malizika.

التفاسير:

external-link copy
18 : 81

وَٱلصُّبۡحِ إِذَا تَنَفَّسَ

Na kwa asubuhi inapo pambazuka, info

Na kwa asubuhi unapo anza mwangaza wake na ukavuma upepo wake,

التفاسير:

external-link copy
19 : 81

إِنَّهُۥ لَقَوۡلُ رَسُولٖ كَرِيمٖ

Kwamba hakika bila ya shaka hii ni kauli ya Mjumbe mtukufu, info

Hakika Qur'ani bila ya shaka ni kauli ya Mjumbe anaye toka kwa Mwenyezi Mungu, naye ni mwenye kuhishimiwa kwake,

التفاسير:

external-link copy
20 : 81

ذِي قُوَّةٍ عِندَ ذِي ٱلۡعَرۡشِ مَكِينٖ

Mwenye nguvu na mwenye cheo kwa huyo Mwenye Kiti cha Enzi, info

Mwenye nguvu katika kutekeleza waajibu wake, mwenye cheo na daraja mbele ya Mwenyezi Mungu Mwenye Kiti cha Enzi.

التفاسير:

external-link copy
21 : 81

مُّطَاعٖ ثَمَّ أَمِينٖ

Anaye t'iiwa, tena muaminifu. info

Tena ni mwenye kut'iiwa, na muaminifu wa kuchukua wahyi miongoni wa walio juu.

التفاسير:

external-link copy
22 : 81

وَمَا صَاحِبُكُم بِمَجۡنُونٖ

Na wala huyu mwenzenu hana wazimu. info

Na huyo Mtume wenu ambaye ni mwenzenu, mnaye mjua kuwa ana akili timamu, si mwendawazimu.

التفاسير:

external-link copy
23 : 81

وَلَقَدۡ رَءَاهُ بِٱلۡأُفُقِ ٱلۡمُبِينِ

Na hakika yeye alimwona kwenye upeo wa macho ulio safi. info

Na ninaapa kuwa Muhammad s.a.w. bila ya shaka alimwona Jibrili katika upeo wa macho kwa mujibu wa inavyo onekana.

التفاسير:

external-link copy
24 : 81

وَمَا هُوَ عَلَى ٱلۡغَيۡبِ بِضَنِينٖ

Wala yeye si bakhili kwa mambo ya ghaibu. info

Na Muhammad si bakhili wa kufikisha wahyi na kuwafunza watu.

التفاسير:

external-link copy
25 : 81

وَمَا هُوَ بِقَوۡلِ شَيۡطَٰنٖ رَّجِيمٖ

Wala hii si kauli ya Shetani maluuni. info

Wala huu wahyi (ufunuo) ulio teremshwa juu yake si kauli ya Shetani aliye fukuzwa kutoka kwenye rehema ya Mwenyezi Mungu.

التفاسير:

external-link copy
26 : 81

فَأَيۡنَ تَذۡهَبُونَ

Basi mnakwenda wapi? info

Basi njia gani iliyo ya uwongofu zaidi kuliko hii mnayo ifuata?

التفاسير:

external-link copy
27 : 81

إِنۡ هُوَ إِلَّا ذِكۡرٞ لِّلۡعَٰلَمِينَ

Haikuwa hii ila ni ukumbusho kwa walimwengu wote. info

Qur'ani si chochote ila ni ukumbusho na mawaidha kwa walimwengu wote.

التفاسير:

external-link copy
28 : 81

لِمَن شَآءَ مِنكُمۡ أَن يَسۡتَقِيمَ

Kwa yule miongoni mwenu anaye taka kwenda sawa. info

Kwa anaye taka, miongoni mwenu, kusimama sawa kufikilia haki na kweli.

التفاسير:

external-link copy
29 : 81

وَمَا تَشَآءُونَ إِلَّآ أَن يَشَآءَ ٱللَّهُ رَبُّ ٱلۡعَٰلَمِينَ

Wala nyinyi hamtataka isipo kuwa atake Mwenyezi Mungu Mola Mlezi wa walimwengu wote. info

Na nyinyi hamwezi kutaka kitu ila anapo taka Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa walimwengu wote.

التفاسير: