పవిత్ర ఖురాన్ యొక్క భావార్థాల అనువాదం - స్వాహిలి అనువాదం - అబ్దుల్లాహ్ ముహమ్మద్ మరియు నాసర్ ఖమీస్

పేజీ నెంబరు:close

external-link copy
41 : 70

عَلَىٰٓ أَن نُّبَدِّلَ خَيۡرٗا مِّنۡهُمۡ وَمَا نَحۡنُ بِمَسۡبُوقِينَ

kuwa Sisi tunaweza kuwaleta watu badala yao walio bora zaidi kuliko wao na watiifu zaidi wa Mwenyezi Mungu. Na hakuna yoyote atakayetushinda na kutuponyoka na kutuelemea iwapo tunataka kumrudisha uhai baada ya kufa. info
التفاسير:

external-link copy
42 : 70

فَذَرۡهُمۡ يَخُوضُواْ وَيَلۡعَبُواْ حَتَّىٰ يُلَٰقُواْ يَوۡمَهُمُ ٱلَّذِي يُوعَدُونَ

Basi waache wavame kwenye ubatilifu wao na wacheze kwenye ulimwengu wao mpaka wakutane na Siku ya Kiyama ambayo wanaahidiwa kuwa wataadhibiwa. info
التفاسير:

external-link copy
43 : 70

يَوۡمَ يَخۡرُجُونَ مِنَ ٱلۡأَجۡدَاثِ سِرَاعٗا كَأَنَّهُمۡ إِلَىٰ نُصُبٖ يُوفِضُونَ

Siku watakapotoka makaburini wakienda kwa haraka, kama wlivyokuwa duniani wakienda mbio na haraka kwa waungu wao wakiwaabudu badala ya Mwenyezi Mungu, info
التفاسير:

external-link copy
44 : 70

خَٰشِعَةً أَبۡصَٰرُهُمۡ تَرۡهَقُهُمۡ ذِلَّةٞۚ ذَٰلِكَ ٱلۡيَوۡمُ ٱلَّذِي كَانُواْ يُوعَدُونَ

hali ya kuwa macho yao ni madhalilifu yanatazama chini, wamefinikwa na unyonge na utwevu. Hiyo ndiyo Siku waliyoahidiwa duniani na walikuwa wakiifanyia shere na kuikanusha. info
التفاسير: