Huwakuti watu wanao msadiki Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho wanapendana na wenye kumfanyia uadui Mwenyezi Mungu na Mtume wake, hata wakiwa ni baba zao, au ni watoto wao, au ni ndugu zao, au ni jamaa zao. Hao ambao hawafanyi urafiki na wanao mpinga Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu ameithibitisha Imani katika nyoyo zao, na amewaunga mkono kwa nguvu zinazo tokana naye Yeye Mwenyewe, na atawatia katika Mabustani yapitayo mito kati yake wakikaa humo milele. Neema zake haziwakatikii. Mwenyezi Mungu amewapenda hao, na wao wamempenda. Hao ndio wanao ambiwa kuwa ni katika Hizbullahi, yaani Kundi la Mwenyezi Mungu. Hakika ni kweli Kundi la Mwenyezi Mungu ndilo lenye kufuzu.