அல்குர்ஆன் மொழிபெயர்ப்பு - சுவாஹிலி மொழிபெயர்ப்பு - அப்துல்லா முஹம்மது மற்றும் நாசர் காமிஸ்

பக்க எண்:close

external-link copy
60 : 6

وَهُوَ ٱلَّذِي يَتَوَفَّىٰكُم بِٱلَّيۡلِ وَيَعۡلَمُ مَا جَرَحۡتُم بِٱلنَّهَارِ ثُمَّ يَبۡعَثُكُمۡ فِيهِ لِيُقۡضَىٰٓ أَجَلٞ مُّسَمّٗىۖ ثُمَّ إِلَيۡهِ مَرۡجِعُكُمۡ ثُمَّ يُنَبِّئُكُم بِمَا كُنتُمۡ تَعۡمَلُونَ

Na Yeye, kutakata na sifa za upungufu ni Kwake, Ndiye Anayezichukua roho zenu usiku kwa namna inayofanana na vile roho hizo zinachukuliwa kipindi cha kifo, na Anayajua matendo mnayoyafanya mchana, kisha Anazirudisha roho zenu kwenye miili yenu kwa kuamka kutoka usingizini kipindi cha mchana kwa namna inayofanana na kuhuisha baada kufa, ili umalizike muda maalumu uliowekwa wa maisha yenu ulimwenguni. Kisha marejeo yenu ni kwa Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, baada ya kufufuliwa kwenu kutoka kwenye makaburi yenu mkiwa hai. Kisha Atawaelezea yale mliokuwa mkiyafanya kipindi cha maisha yenu ya ulimengu. Kisha Atawalipa kwa hayo. info
التفاسير:

external-link copy
61 : 6

وَهُوَ ٱلۡقَاهِرُ فَوۡقَ عِبَادِهِۦۖ وَيُرۡسِلُ عَلَيۡكُمۡ حَفَظَةً حَتَّىٰٓ إِذَا جَآءَ أَحَدَكُمُ ٱلۡمَوۡتُ تَوَفَّتۡهُ رُسُلُنَا وَهُمۡ لَا يُفَرِّطُونَ

Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, Ndiye Al-Qāhir (Mtendesha nguvu), Aliye juu ya waja Wake, ujuu wa kila namana usio na mipaka unaonasibiana na utkufu Wake, kutakata na kila sifa mbaya ni Kwake na kutukuka ni Kwake. Kila kitu kinaunyenyekea utukufu Wake na ukubwa Wake. Yeye Anawatuma kwa waja Wake Malaika kuyadhibiti matendo yao na kuyahesabu. Mpaka kifo kinapomshukia mmoja wao, Malaika wa mauti na wasaidizi wake wanaichukua roho yake, na wao hawaachi kutekeleza walichoamrishwa kukifanya. info
التفاسير:

external-link copy
62 : 6

ثُمَّ رُدُّوٓاْ إِلَى ٱللَّهِ مَوۡلَىٰهُمُ ٱلۡحَقِّۚ أَلَا لَهُ ٱلۡحُكۡمُ وَهُوَ أَسۡرَعُ ٱلۡحَٰسِبِينَ

Kisha hawa waliokufa watarudishwa kwa Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, Mola wao wa kweli. Jua utanabahi kwamba hukumu na uamuzi baina ya waja Wake, Siku ya Kiyama, ni Vyake Yeye tu. Na Yeye Ndiye Mwpesi wa wenye kuhesabu. info
التفاسير:

external-link copy
63 : 6

قُلۡ مَن يُنَجِّيكُم مِّن ظُلُمَٰتِ ٱلۡبَرِّ وَٱلۡبَحۡرِ تَدۡعُونَهُۥ تَضَرُّعٗا وَخُفۡيَةٗ لَّئِنۡ أَنجَىٰنَا مِنۡ هَٰذِهِۦ لَنَكُونَنَّ مِنَ ٱلشَّٰكِرِينَ

Waambie, ewe Mtume, hawa washirikina, «Ni nani mwenye kuwaokoa na vitisho vya magiza ya bara na bahari? Kwani si Mwenyezi Mungu mnayemuomba kwenye matatizo mkionesha unyonge wenu kwa dhahiri na kwa siri? Huwa mkisema, ‘Hakika Mola wetu Akituokoa na vitisho hivi, tutakuwa ni wenye kushukuru kwa kumuabudu, Aliyeshinda na kutukuka, Peke Yake, Asiye na mshirika.» info
التفاسير:

external-link copy
64 : 6

قُلِ ٱللَّهُ يُنَجِّيكُم مِّنۡهَا وَمِن كُلِّ كَرۡبٖ ثُمَّ أَنتُمۡ تُشۡرِكُونَ

Waambie, ewe Mtume, «Mwenyezi Mungu, Peke Yake, Ndiye Mwenye kuwaokoa na vitisho hivyi na kila tatizo, kisha nyinyi baada ya hapo mnawashirikisha wengine pamoja Naye katika ibada.» info
التفاسير:

external-link copy
65 : 6

قُلۡ هُوَ ٱلۡقَادِرُ عَلَىٰٓ أَن يَبۡعَثَ عَلَيۡكُمۡ عَذَابٗا مِّن فَوۡقِكُمۡ أَوۡ مِن تَحۡتِ أَرۡجُلِكُمۡ أَوۡ يَلۡبِسَكُمۡ شِيَعٗا وَيُذِيقَ بَعۡضَكُم بَأۡسَ بَعۡضٍۗ ٱنظُرۡ كَيۡفَ نُصَرِّفُ ٱلۡأٓيَٰتِ لَعَلَّهُمۡ يَفۡقَهُونَ

Sema, ewe Mtume, «Mwenyezi Mungu, Aliyeshinda na kutukuka, Ndiye Muweza, Peke Yake, kuwatumia adhabu kutoka juu yenu, kama kupigwa majiwe au mvua ya mafuriko na mfano wake, au kutoka chini ya miguu yenu, kama mitetemeko ya ardhi na kuzama ndani ardhi, au Awavurugie mambo yenu muwe makundi yanayozozana, mnauana nyinyi kwa nyinyi,» Angalia, ewe Mtume, vipi tunazifanya aina mbalimbali hoja zetu zilizo wazi kwa hawa washirikina ili waelewe na wazingatie! info
التفاسير:

external-link copy
66 : 6

وَكَذَّبَ بِهِۦ قَوۡمُكَ وَهُوَ ٱلۡحَقُّۚ قُل لَّسۡتُ عَلَيۡكُم بِوَكِيلٖ

Na waliikanusha hii Qur’ani makafiri kati ya watu wako, ewe Mtume; nayo ni kitabu chenye ukweli katika kila kilichokuja nacho, Waambie, «Mimi si mlinzi wala mtunzi juuu yenu. Mimi ni mjumbe wa Mwenyezi Mungu, nawafikishia nyinyi yale niliotumwa nayo kwenu,. info
التفاسير:

external-link copy
67 : 6

لِّكُلِّ نَبَإٖ مُّسۡتَقَرّٞۚ وَسَوۡفَ تَعۡلَمُونَ

Kila habari ina kituo cha kutulia na kikomo cha kukomea, hapo haki na batili zitafunuka. Na mtajua, enyi makafiri, mwisho wa jambo lenu, itakaposhuka adhabu ya Mwenyezi Mungu kwenu. info
التفاسير:

external-link copy
68 : 6

وَإِذَا رَأَيۡتَ ٱلَّذِينَ يَخُوضُونَ فِيٓ ءَايَٰتِنَا فَأَعۡرِضۡ عَنۡهُمۡ حَتَّىٰ يَخُوضُواْ فِي حَدِيثٍ غَيۡرِهِۦۚ وَإِمَّا يُنسِيَنَّكَ ٱلشَّيۡطَٰنُ فَلَا تَقۡعُدۡ بَعۡدَ ٱلذِّكۡرَىٰ مَعَ ٱلۡقَوۡمِ ٱلظَّٰلِمِينَ

Na uwaonapo, ewe Mtume, washirikina wanaoleta maneno juu ya aya za Qur’ani, kwa urongo na kwa kufanya shere, jiepushe na wao mpaka waingie kwenye maneno mengine. Na iwapo Shetani amekusahaulisha jambo hili, basi baada ya kukumbuka usikae pamoja na watu wenye uadui walioleta maneno ya urongo juu ya aya za Mwenyezi Mungu, info
التفاسير: