அல்குர்ஆன் மொழிபெயர்ப்பு - சுவாஹிலி மொழிபெயர்ப்பு - அப்துல்லா முஹம்மது மற்றும் நாசர் காமிஸ்

பக்க எண்:close

external-link copy
57 : 39

أَوۡ تَقُولَ لَوۡ أَنَّ ٱللَّهَ هَدَىٰنِي لَكُنتُ مِنَ ٱلۡمُتَّقِينَ

«Au ikasema, ‘Lau Mwenyezi Mungu Angaliniongoza kwenye Dini Yake ningalikuwa ni miongoni mwa wenye kujikinga na ushirikina na maasia.’» info
التفاسير:

external-link copy
58 : 39

أَوۡ تَقُولَ حِينَ تَرَى ٱلۡعَذَابَ لَوۡ أَنَّ لِي كَرَّةٗ فَأَكُونَ مِنَ ٱلۡمُحۡسِنِينَ

«Au ikasema, itakapo kuiona adhabu ya Mwenyezi Mungu imeizunguka Siku ya Kiyama, ‘Natamani nipatiwe nafasi ya kurudi kwenye maisha ya kilimwengu nikawa huko ni miongoni mwa wenye kufanya wema kwa kumtii Mola wao na kufanya matendo yaliyoamrishwa na Mitume.’» info
التفاسير:

external-link copy
59 : 39

بَلَىٰ قَدۡ جَآءَتۡكَ ءَايَٰتِي فَكَذَّبۡتَ بِهَا وَٱسۡتَكۡبَرۡتَ وَكُنتَ مِنَ ٱلۡكَٰفِرِينَ

Maneno siyo kama unavyosema, Kwa hakika aya zangu zilizo wazi zenye kuitolea ushahidi haki zilikujia ukazikanusha, ukazifanyia kiburi usizikubali na usizifuate na ukawa ni miongoni mwa wenye kumkanusha Mwenyezi Mungu na Mitume Wake. info
التفاسير:

external-link copy
60 : 39

وَيَوۡمَ ٱلۡقِيَٰمَةِ تَرَى ٱلَّذِينَ كَذَبُواْ عَلَى ٱللَّهِ وُجُوهُهُم مُّسۡوَدَّةٌۚ أَلَيۡسَ فِي جَهَنَّمَ مَثۡوٗى لِّلۡمُتَكَبِّرِينَ

Na Siku ya Kiyama utawaona hao wakanushaji, waliomsifu Mola wao kwa sifa zisizolingana na Yeye na wakamnasibisha Yeye na mshirika na mwana, nyuso zao zimekuwa nyeusi. Si ndani ya Jahanamu kuna mashukio na makao kwa aliyemfanyia Mwenyezi Mungu kiburi akakataa kumpwekesha na kumtii? Ndio. info
التفاسير:

external-link copy
61 : 39

وَيُنَجِّي ٱللَّهُ ٱلَّذِينَ ٱتَّقَوۡاْ بِمَفَازَتِهِمۡ لَا يَمَسُّهُمُ ٱلسُّوٓءُ وَلَا هُمۡ يَحۡزَنُونَ

Na Mwenyezi Mungu Atawaokoa na Moto wa Jahanamu na adhabu yake wale waliomcha Mola wao kwa kutekeleza faradhi Alizoziamrisha na kujiepusha na yale Aliyoyakataza kwa kufuzu kwao na kutimia matakwa yao, nako ni kufaulu kupata Pepo. Hawataguswa na kitu chochote cha adhabu wala hawatazisikitikia hadhi za duniani walizozikosa. info
التفاسير:

external-link copy
62 : 39

ٱللَّهُ خَٰلِقُ كُلِّ شَيۡءٖۖ وَهُوَ عَلَىٰ كُلِّ شَيۡءٖ وَكِيلٞ

Mwenyezi Mungu Aliyetukuka Ndiye Muumba wa vitu vyote, Ndiye Mola wa hivyo vitu na Ndiye Mwenye kuviendesha. Na Yeye ni Mtunzi wa kila kitu. Anayaendesha mambo yote ya viumbe Vyake. info
التفاسير:

external-link copy
63 : 39

لَّهُۥ مَقَالِيدُ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِۗ وَٱلَّذِينَ كَفَرُواْ بِـَٔايَٰتِ ٱللَّهِ أُوْلَٰٓئِكَ هُمُ ٱلۡخَٰسِرُونَ

Ni za Mwenyezi Mungu funguo za hazina za mbinguni na ardhini, Anatoa kutoka kwenye hazina hizo kuwapa viumbe Vyake namna Anavyotaka. Na wale waliozikanusha aya za Qur’ani na dalili wazi zilizomo, hao ndio wenye kupata hasara ulimwenguni kwa kutoafikiwa kuamini, na kesho Akhera kwa kukaa milele Motoni. info
التفاسير:

external-link copy
64 : 39

قُلۡ أَفَغَيۡرَ ٱللَّهِ تَأۡمُرُوٓنِّيٓ أَعۡبُدُ أَيُّهَا ٱلۡجَٰهِلُونَ

Sema, ewe Mtume, uwaambie washirikina wa watu wako, «Je, yule asiyekuwa Mwenyezi Mungu, enyi wajinga, mnanishauri nimuabudu na hali ibada haifai kufanyiwa kitu chochote isipokuwa Yeye?» info
التفاسير:

external-link copy
65 : 39

وَلَقَدۡ أُوحِيَ إِلَيۡكَ وَإِلَى ٱلَّذِينَ مِن قَبۡلِكَ لَئِنۡ أَشۡرَكۡتَ لَيَحۡبَطَنَّ عَمَلُكَ وَلَتَكُونَنَّ مِنَ ٱلۡخَٰسِرِينَ

Kwa hakika uliletewa wahyi wewe, ewe Mtume, na Mitume waliokuwa kabla yako kwamba lau ulimshirikisha Mwenyezi Mungu na asiyekuwa Yeye amali zako zingalibatilika na ungalikuwa ni miongoni mwa walioangamia waliopata hasara, hivyo basi ukapata hasara ya dini yako na Akhera Yako, kwani pamoja na ushirikina haikubaliwi amali njema. info
التفاسير:

external-link copy
66 : 39

بَلِ ٱللَّهَ فَٱعۡبُدۡ وَكُن مِّنَ ٱلشَّٰكِرِينَ

Bali Mwenyezi Mungu muabudu, ewe Mtume, kwa kumtakasia ibada Peke Yake Asiye na mshirika, na uwe ni miongoni mwa wenye kuzishukuru neema za Mwenyezi Mungu. info
التفاسير:

external-link copy
67 : 39

وَمَا قَدَرُواْ ٱللَّهَ حَقَّ قَدۡرِهِۦ وَٱلۡأَرۡضُ جَمِيعٗا قَبۡضَتُهُۥ يَوۡمَ ٱلۡقِيَٰمَةِ وَٱلسَّمَٰوَٰتُ مَطۡوِيَّٰتُۢ بِيَمِينِهِۦۚ سُبۡحَٰنَهُۥ وَتَعَٰلَىٰ عَمَّا يُشۡرِكُونَ

Na hawa washirikina hawakumuadhimisha Mwenyezi Mungu vile Anavyostahiki kuadhimishwa, kwa kuwa wamemuabudu asiyekuwa Yeye pamoja na Yeye miongoni mwa wale wasionufaisha wala kudhuru, wakamfanya muumbwa, pamoja na uelemevu wake, kuwa ni sawa na Muumba Mtukufu, Ambaye kotokana na uweza Wake mkubwa ni kwamba ardhi yote itakuwa iko mkononi Mwake Siku ya Kiyama, na mbingu zitakuwa zimekunjwa kwa mkono Wake wa kulia. Ametakasika Mwenyezi Mungu na kutukuka kwa kuepukana na kile wanaomshirikisha nacho hao washirikina. Katika aya hii pana dalili ya kuthibitisha kushika kwa mkono, mkono wa kulia na kukunja kwa Mwenyezi Mungu kama vile inavyolingana na haiba Yake na utukufu Wake bila kueleza Yuko vipi wala kufananisha. info
التفاسير: