د قرآن کریم د معناګانو ژباړه - سواحلي ژباړه - د رواد الترجمې مرکز

د مخ نمبر:close

external-link copy
36 : 69

وَلَا طَعَامٌ إِلَّا مِنۡ غِسۡلِينٖ

Wala hana chakula ila usaha wa watu wa Motoni. info
التفاسير:

external-link copy
37 : 69

لَّا يَأۡكُلُهُۥٓ إِلَّا ٱلۡخَٰطِـُٔونَ

Chakula hicho hawakili ila wakosefu. info
التفاسير:

external-link copy
38 : 69

فَلَآ أُقۡسِمُ بِمَا تُبۡصِرُونَ

Basi ninaapa kwa mnavyoviona. info
التفاسير:

external-link copy
39 : 69

وَمَا لَا تُبۡصِرُونَ

Na msivyoviona. info
التفاسير:

external-link copy
40 : 69

إِنَّهُۥ لَقَوۡلُ رَسُولٖ كَرِيمٖ

Kwa hakika hii ni kauli iliyoletwa na Mjumbe mwenye heshima. info
التفاسير:

external-link copy
41 : 69

وَمَا هُوَ بِقَوۡلِ شَاعِرٖۚ قَلِيلٗا مَّا تُؤۡمِنُونَ

Wala si kauli ya mtunga mashairi. Ni machache sana mnayoyaamini. info
التفاسير:

external-link copy
42 : 69

وَلَا بِقَوۡلِ كَاهِنٖۚ قَلِيلٗا مَّا تَذَكَّرُونَ

Wala si kauli ya kuhani. Ni machache mnayoyakumbuka. info
التفاسير:

external-link copy
43 : 69

تَنزِيلٞ مِّن رَّبِّ ٱلۡعَٰلَمِينَ

Ni uteremsho utokao kwa Mola Mlezi wa walimwengu wote. info
التفاسير:

external-link copy
44 : 69

وَلَوۡ تَقَوَّلَ عَلَيۡنَا بَعۡضَ ٱلۡأَقَاوِيلِ

Na lau kama angelituzulia baadhi ya maneno tu. info
التفاسير:

external-link copy
45 : 69

لَأَخَذۡنَا مِنۡهُ بِٱلۡيَمِينِ

Bila ya shaka tungelimshika kwa mkono wa kulia. info
التفاسير:

external-link copy
46 : 69

ثُمَّ لَقَطَعۡنَا مِنۡهُ ٱلۡوَتِينَ

Kisha kwa hakika tungelimkata mshipa mkubwa wa moyo! info
التفاسير:

external-link copy
47 : 69

فَمَا مِنكُم مِّنۡ أَحَدٍ عَنۡهُ حَٰجِزِينَ

Na hapana yeyote katika nyinyi ambaye angeliweza kutuzuia. info
التفاسير:

external-link copy
48 : 69

وَإِنَّهُۥ لَتَذۡكِرَةٞ لِّلۡمُتَّقِينَ

Kwa hakika hii ni mawaidha kwa wacha Mungu. info
التفاسير:

external-link copy
49 : 69

وَإِنَّا لَنَعۡلَمُ أَنَّ مِنكُم مُّكَذِّبِينَ

Na hakika Sisi bila ya shaka tunajua kwamba miongoni mwenu wapo wanaokadhibisha. info
التفاسير:

external-link copy
50 : 69

وَإِنَّهُۥ لَحَسۡرَةٌ عَلَى ٱلۡكَٰفِرِينَ

Na hakika bila ya shaka itakuwa ni majuto kwa wanaokataa. info
التفاسير:

external-link copy
51 : 69

وَإِنَّهُۥ لَحَقُّ ٱلۡيَقِينِ

Na hakika hii bila ya shaka ni haki ya yakini. info
التفاسير:

external-link copy
52 : 69

فَسَبِّحۡ بِٱسۡمِ رَبِّكَ ٱلۡعَظِيمِ

Basi litakase jina la Mola wako Mlezi Mtukufu. info
التفاسير: