د قرآن کریم د معناګانو ژباړه - سواحلي ژباړه - د رواد الترجمة مرکز

د مخ نمبر:close

external-link copy
74 : 6

۞ وَإِذۡ قَالَ إِبۡرَٰهِيمُ لِأَبِيهِ ءَازَرَ أَتَتَّخِذُ أَصۡنَامًا ءَالِهَةً إِنِّيٓ أَرَىٰكَ وَقَوۡمَكَ فِي ضَلَٰلٖ مُّبِينٖ

Na pale Ibrahim alipomwambia baba yake, Azar: Unayafanya masanamu kuwa ni miungu? Hakika mimi nakuona wewe na watu wako mko katika upotovu ulio wazi. info
التفاسير:

external-link copy
75 : 6

وَكَذَٰلِكَ نُرِيٓ إِبۡرَٰهِيمَ مَلَكُوتَ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِ وَلِيَكُونَ مِنَ ٱلۡمُوقِنِينَ

Na vivyo hivyo tulimwonyesha Ibrahim ufalme wa mbingu na ardhi, na ili awe miongoni mwa wenye yakini. info
التفاسير:

external-link copy
76 : 6

فَلَمَّا جَنَّ عَلَيۡهِ ٱلَّيۡلُ رَءَا كَوۡكَبٗاۖ قَالَ هَٰذَا رَبِّيۖ فَلَمَّآ أَفَلَ قَالَ لَآ أُحِبُّ ٱلۡأٓفِلِينَ

Na ulipomwingilia usiku, aliona nyota kubwa, akasema: Huyu ndiye Mola wangu Mlezi. Na ilipotua, akasema: Siwapendi wanaotua. info
التفاسير:

external-link copy
77 : 6

فَلَمَّا رَءَا ٱلۡقَمَرَ بَازِغٗا قَالَ هَٰذَا رَبِّيۖ فَلَمَّآ أَفَلَ قَالَ لَئِن لَّمۡ يَهۡدِنِي رَبِّي لَأَكُونَنَّ مِنَ ٱلۡقَوۡمِ ٱلضَّآلِّينَ

Alipouona mwezi unachomoza alisema: Huyu ndiye Mola wangu Mlezi. Na ulipotua, akasema: Kama Mola wangu Mlezi hataniongoa, basi hakika nitakuwa miongoni mwa kaumu waliopotea. info
التفاسير:

external-link copy
78 : 6

فَلَمَّا رَءَا ٱلشَّمۡسَ بَازِغَةٗ قَالَ هَٰذَا رَبِّي هَٰذَآ أَكۡبَرُۖ فَلَمَّآ أَفَلَتۡ قَالَ يَٰقَوۡمِ إِنِّي بَرِيٓءٞ مِّمَّا تُشۡرِكُونَ

Na alipoliona jua linachomoza, akasema: 'Huyu ndiye Mola wangu Mlezi. Huyu ni mkubwa zaidi.' Na lilipotua, akasema: Enyi kaumu yangu! Mimi niko mbali sana na hayo mnayoshirikisha. info
التفاسير:

external-link copy
79 : 6

إِنِّي وَجَّهۡتُ وَجۡهِيَ لِلَّذِي فَطَرَ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضَ حَنِيفٗاۖ وَمَآ أَنَا۠ مِنَ ٱلۡمُشۡرِكِينَ

Hakika mimi nimeuelekeza uso wangu kwa yule aliyeziumba mbingu na ardhi, huku nikiwa mnyoofu, wala mimi si miongoni mwa washirikina. info
التفاسير:

external-link copy
80 : 6

وَحَآجَّهُۥ قَوۡمُهُۥۚ قَالَ أَتُحَٰٓجُّوٓنِّي فِي ٱللَّهِ وَقَدۡ هَدَىٰنِۚ وَلَآ أَخَافُ مَا تُشۡرِكُونَ بِهِۦٓ إِلَّآ أَن يَشَآءَ رَبِّي شَيۡـٔٗاۚ وَسِعَ رَبِّي كُلَّ شَيۡءٍ عِلۡمًاۚ أَفَلَا تَتَذَكَّرُونَ

Na kaumu yake wakamhoji. Akasema: Je, mnanihoji kuhusiana na Mwenyezi Mungu, na ilhali Yeye hakika amekwishaniongoa? Wala siogopi hao mnaowashirikisha naye, isipokuwa ikiwa Mola wangu Mlezi akipenda kitu. Mola wangu Mlezi amekusanya elimu ya kila kitu. Basi je, hamkumbuki? info
التفاسير:

external-link copy
81 : 6

وَكَيۡفَ أَخَافُ مَآ أَشۡرَكۡتُمۡ وَلَا تَخَافُونَ أَنَّكُمۡ أَشۡرَكۡتُم بِٱللَّهِ مَا لَمۡ يُنَزِّلۡ بِهِۦ عَلَيۡكُمۡ سُلۡطَٰنٗاۚ فَأَيُّ ٱلۡفَرِيقَيۡنِ أَحَقُّ بِٱلۡأَمۡنِۖ إِن كُنتُمۡ تَعۡلَمُونَ

Na vipi nivihofu hivyo mlivyovishirikisha, ilhali nyinyi hamhofu kuwa nyinyi mmemshirikisha Mwenyezi Mungu na kitu ambacho hakuwateremshia uthibitisho juu yake. Basi ni kundi gani katika mawili haya lina haki zaidi kupata amani, ikiwa nyinyi mnajua? info
التفاسير: