د قرآن کریم د معناګانو ژباړه - سواحلي ژباړه - د رواد الترجمة مرکز

external-link copy
83 : 2

وَإِذۡ أَخَذۡنَا مِيثَٰقَ بَنِيٓ إِسۡرَٰٓءِيلَ لَا تَعۡبُدُونَ إِلَّا ٱللَّهَ وَبِٱلۡوَٰلِدَيۡنِ إِحۡسَانٗا وَذِي ٱلۡقُرۡبَىٰ وَٱلۡيَتَٰمَىٰ وَٱلۡمَسَٰكِينِ وَقُولُواْ لِلنَّاسِ حُسۡنٗا وَأَقِيمُواْ ٱلصَّلَوٰةَ وَءَاتُواْ ٱلزَّكَوٰةَ ثُمَّ تَوَلَّيۡتُمۡ إِلَّا قَلِيلٗا مِّنكُمۡ وَأَنتُم مُّعۡرِضُونَ

Na tulipofunga agano na Wana wa Israili: Hamtamuabudu yeyote ila Mwenyezi Mungu; na muwafanyie wema wazazi na jamaa na mayatima na masikini, na semeni na watu kwa wema, na shikeni Swala, na toeni Zaka. Kisha mkageuka isipokuwa wachache tu katika nyinyi; na nyinyi mnapuuza.[1] info

[1] Mwenyezi Mungu aliwaamrisha kuwafanyia wema wazazi, na akaunganisha katika Aya hii haki ya wazazi na tawhidi, kwa sababu malezi ya kwanza yalitoka kwa Mwenyezi Mungu, na malezi ya pili yanatoka kwa wazazi. (Tafsir Al-Qurtubii)

التفاسير: