a mliposema: Ewe Musa! Hatuwezi kuvumilia chakula cha namna moja tu, basi tuombee kwa Mola wako Mlezi atutolee vile vinavyomea katika Ardhi, kama mboga zake, na matango yake, na thom zake, na adesi zake, na vitunguu vyake. Akasema: Mnabadili kilicho duni kwa kilicho bora? Shukeni mjini, huko mtapata mlivyoviomba. Na wakapigwa na unyonge,na umasikini, na wakastahili ghadhabu ya Mwenyezi Mungu. Na haya ni kwa sababu walikuwa wakiyakataa maneno ya Mwenyezi Mungu, na wakiwauwa Manabii pasipo haki. Hayo ni kwa walivyoasi na wakapindukia mipaka.[1]
[1] Hapa kuna tishio kwa umma huu kwa wale wanaoitaka dunia sana ambao huchagua vilivyo chini, yani vilivyo haramu, na kuacha vile vilivyo juu, yani halali, ili wasije wakawa kama hao wana wa Israil . (Tafsir Al-Biqaa'ii)