د قرآن کریم د معناګانو ژباړه - سواحلي ژباړه - د رواد الترجمة مرکز

external-link copy
16 : 2

أُوْلَٰٓئِكَ ٱلَّذِينَ ٱشۡتَرَوُاْ ٱلضَّلَٰلَةَ بِٱلۡهُدَىٰ فَمَا رَبِحَت تِّجَٰرَتُهُمۡ وَمَا كَانُواْ مُهۡتَدِينَ

Hao ndio walioununua upotovu kwa uwongofu; lakini biashara yao haikupata faida, wala hawakuwa wenye kuongoka.[1] info

[1] Na huu ni katika mifano mizuri kabisa. Kwani (mnafiki) aliufanya upotovu ambao ndio shari kubwa zaidi kuwa bidhaa, na akaufanya uwongofu ambao ndio kutengenea kukubwa zaidi pahali pa bei. Kwa hivyo, wakautoa uwongofu (ambayo ndiyo bei) kwa kuukataa na kuutaka upotovu (ambayo ndiyo bidhaa). (Tafsir Assa'dii) Lakini biashara hiyo yao haikupata faida, pamoja na kudai kwao kwamba wao ndio wajuzi zaidi katika hilo la kutengeneza. Na wala hawakuongoka, yaani walipoteza mpaka mtaji wao, yani uwongofu wa Qur-aani. (Tafsir Nidhaam Addurar fii Tanasub Al-Aayat Wassuwar cha Al-Baqaa'ii)

التفاسير: