د قرآن کریم د معناګانو ژباړه - سواحلي ژباړه - د رواد الترجمة مرکز

external-link copy
133 : 2

أَمۡ كُنتُمۡ شُهَدَآءَ إِذۡ حَضَرَ يَعۡقُوبَ ٱلۡمَوۡتُ إِذۡ قَالَ لِبَنِيهِ مَا تَعۡبُدُونَ مِنۢ بَعۡدِيۖ قَالُواْ نَعۡبُدُ إِلَٰهَكَ وَإِلَٰهَ ءَابَآئِكَ إِبۡرَٰهِـۧمَ وَإِسۡمَٰعِيلَ وَإِسۡحَٰقَ إِلَٰهٗا وَٰحِدٗا وَنَحۡنُ لَهُۥ مُسۡلِمُونَ

Je, mlikuwapo yalipomfikia Yaaqub mauti, akawaambia wanawe: Mtamuabudu nani baada yangu? Wakasema: Tutamuabudu Mungu wako na Mungu wa baba zako, Ibrahim na Ismail na Is-hak, Mungu Mmoja tu. Na sisi tunasilimu kwake.[1] info

[1] Hii ni hoja dhidi ya Mayahudi (na mfano wao) wanaodai kuwa wanaifuata mila (dini) ya Ibrahim na (Manabii wa) baada yake (kama vile) Yaaqub. Mwenyezi Mungu Mtukufu akawauliza ikiwa waliushuhudia wasia wa mwisho wa Yaqub kwa wana wake. "Je, mtamuabudu nani baada yangu?" Wakasema kuwa watamuabudu Mungu wake, Mungu wa baba zake, ambaye ni Mungu Mmoja tu, na kwamba wao ni wenye kujisilimisha kwake (yani Waislamu)." (Tafsir Assa'dii)

التفاسير: