د قرآن کریم د معناګانو ژباړه - سواحلي ژباړه - علی محسن البرواني

external-link copy
12 : 2

أَلَآ إِنَّهُمۡ هُمُ ٱلۡمُفۡسِدُونَ وَلَٰكِن لَّا يَشۡعُرُونَ

Hakika wao ndio waharibifu, lakini hawatambui. info

Enyi Waumini! Amkeni, mtanabahi, muwatambue kuwa hao ndio mafisadi wa kweli, lakini wenyewe hawautambui ufisadi wao kwa ajili ya ghururi walio nayo, wala hawaitambui adhabu kali watakayo ipata kwa unaafiki wao huu.

التفاسير: