د قرآن کریم د معناګانو ژباړه - سواحلي ژباړه - علی محسن البرواني

external-link copy
100 : 2

أَوَكُلَّمَا عَٰهَدُواْ عَهۡدٗا نَّبَذَهُۥ فَرِيقٞ مِّنۡهُمۚ بَلۡ أَكۡثَرُهُمۡ لَا يُؤۡمِنُونَ

Je! Ati ndio kila wanapo funga ahadi huwapo kikundi miongoni mwao kikaivunja? Bali wengi wao hawaamini. info

Na kama (hawa Wana wa Israili) walivyo kuwa vigeugeu katika itikadi na imani, hali kadhaalika walikuwa vigeugeu katika ahadi na mapatano wanayo choka nayo. Walikuwa kila wanapo fungamana na Waislamu au wengineo kwa maagano hutokea kikundi miongoni mwao wakavunjilia mbali maagano hayo. Kwani wengi wao hawaamini utukufu wa ahadi na utakatifu wa maagano.

التفاسير: