د قرآن کریم د معناګانو ژباړه - سواحلي ژباړه - عبد الله محمد او ناصر خمیس

Al-Infitar

external-link copy
1 : 82

إِذَا ٱلسَّمَآءُ ٱنفَطَرَتۡ

Pindi mbingu zitakapopasuka na ukaharibika mpango wake. info
التفاسير:

external-link copy
2 : 82

وَإِذَا ٱلۡكَوَاكِبُ ٱنتَثَرَتۡ

Na pindi nyota zitakapoangukiana. info
التفاسير:

external-link copy
3 : 82

وَإِذَا ٱلۡبِحَارُ فُجِّرَتۡ

Na pindi Mwenyezi Mungu Atakapozifanya bahari kulipuka na maji yake kutoweka. info
التفاسير:

external-link copy
4 : 82

وَإِذَا ٱلۡقُبُورُ بُعۡثِرَتۡ

Na pindi makaburi yatakapogeuzwa kwa kufufuliwa waliokuwamo ndani yake. info
التفاسير:

external-link copy
5 : 82

عَلِمَتۡ نَفۡسٞ مَّا قَدَّمَتۡ وَأَخَّرَتۡ

Wakati huo itajua kila nafsi vitendo vyake vyote ilivyovifanya, vilivyotangulia na vilivyoahirika na italipwa kwa vitendo hivyo. info
التفاسير:

external-link copy
6 : 82

يَٰٓأَيُّهَا ٱلۡإِنسَٰنُ مَا غَرَّكَ بِرَبِّكَ ٱلۡكَرِيمِ

Ewe binadamu unayekanusha kufufuliwa! Ni kipi kilichokufanya uhadaike na ughurike kuhusu Mola wako Mpaji Mwenye kheri nyingi, Anayestahiki kushukuriwa na kutiiwa? info
التفاسير:

external-link copy
7 : 82

ٱلَّذِي خَلَقَكَ فَسَوَّىٰكَ فَعَدَلَكَ

Kwani si Yeye Aliyekuumba, Akalisawazisha umbo lako, Akakuweka katika hali ya sawa na Akakurekibisha ili uweze kutekeleza nyadhifa zako, info
التفاسير:

external-link copy
8 : 82

فِيٓ أَيِّ صُورَةٖ مَّا شَآءَ رَكَّبَكَ

katika sura yoyote ile Aliyoitaka Akakuumba? info
التفاسير:

external-link copy
9 : 82

كَلَّا بَلۡ تُكَذِّبُونَ بِٱلدِّينِ

Mambo hayako kama vile mnavyosema kwamba nyinyi mna haki ya kumuabudu asiyekuwa Mwenyezi Mungu. Bali nyinyi mnaikanusha Siku ya Hesabu na Malipo. info
التفاسير:

external-link copy
10 : 82

وَإِنَّ عَلَيۡكُمۡ لَحَٰفِظِينَ

Na mjue kuwa wako na nyinyi Malaika wachunguzi, info
التفاسير:

external-link copy
11 : 82

كِرَامٗا كَٰتِبِينَ

watukufu kwa Mwenyezi Mungu, waandishi wa yale waliyowakilishwa kuyadhibiti. Hakiwapiti, katika vitendo vyenu na siri zenu, chochote. info
التفاسير:

external-link copy
12 : 82

يَعۡلَمُونَ مَا تَفۡعَلُونَ

Wanayajua mnayoyafanya, ya kheri au ya shari. info
التفاسير:

external-link copy
13 : 82

إِنَّ ٱلۡأَبۡرَارَ لَفِي نَعِيمٖ

Hakika wachamungu wanaotekeleza haki za Mwenyezi Mungu na haki za waja wake watakuwa kwenye neema. info
التفاسير:

external-link copy
14 : 82

وَإِنَّ ٱلۡفُجَّارَ لَفِي جَحِيمٖ

Hakika watu waovu waliopuuza haki za Mwenyezi Mungu na haki za waja wake watakuwa katika Moto mkali. info
التفاسير:

external-link copy
15 : 82

يَصۡلَوۡنَهَا يَوۡمَ ٱلدِّينِ

Ukali wake, Moto huo, utawapata Siku ya Malipo.Na wala wao hawatakuwa ni wenye kughibu, info
التفاسير:

external-link copy
16 : 82

وَمَا هُمۡ عَنۡهَا بِغَآئِبِينَ

wakawa hawamo ndani ya Moto wa Jahanamu, si kwa kutoka wala kwa kufa. info
التفاسير:

external-link copy
17 : 82

وَمَآ أَدۡرَىٰكَ مَا يَوۡمُ ٱلدِّينِ

Ni kipi kinachokujuza ni upi utukufu wa Siku ya Hesabu? info
التفاسير:

external-link copy
18 : 82

ثُمَّ مَآ أَدۡرَىٰكَ مَا يَوۡمُ ٱلدِّينِ

Kisha ni kipi kinachokujuza ni upi utukufu wa Siku ya Hesabu? info
التفاسير:

external-link copy
19 : 82

يَوۡمَ لَا تَمۡلِكُ نَفۡسٞ لِّنَفۡسٖ شَيۡـٔٗاۖ وَٱلۡأَمۡرُ يَوۡمَئِذٖ لِّلَّهِ

Siku ya Hesabu, hataweza yoyote kumnufaisha yoyote. Na amri zote Siku Hiyo ni za Mwenyezi Mungu Peke yake Ambaye hakuna mwenye kumshinda, wala hakuna mwenye kumtendesha nguvu, wala hakuna mwenye kushindana na Yeye. info
التفاسير: